Pata taarifa kuu

Niger: Ecowas yapinga mpango wa jeshi kuhusu kipindi cha mpito

Nairobi – Jumuiya ya Ecowas imepinga mpango wa uongozi wa kijeshi nchini Niger kurejesha utawala wa kiraia nchini humo baada ya kipindi cha miaka mitatu.

Kwamishinan harkokin siyasa, zaman lafiya da tsaro na kungiyar ECOWAS, Abdel-Fatau Musah.
Kwamishinan harkokin siyasa, zaman lafiya da tsaro na kungiyar ECOWAS, Abdel-Fatau Musah. REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kamishena wa masuala ya kisiasa katika Jumuiya hiyo ya Ecowas, Abdel-Fatau Musa, mpango huo haukubaliki.

Jumamosi ya wiki iliyopita, mkuu wa uongozi wa kijeshi nchini Niger Jenerali Abdourahamane Tchiani alisema ratiba hiyo ya serikali ya mpito inalenga kuweka msingi wa mpangilio mpya wa kisiasa nchini humo.

Jenerali Abdourahamane Tiani- Kiongozi wa kijeshi nchini Niger
Jenerali Abdourahamane Tiani- Kiongozi wa kijeshi nchini Niger AP

Ecowas imeitishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia wa rais aliyeondolewa kupitia mapinduzi ya kijeshi.

Haya yanajiri wakati huu maelfu ya raia wa Niger, Jumapili ya wiki hii wakiandamana jijini Niamey, kuunga mkono uongozi wa jeshi, ulomwondoa madarakani, rais Mohammed Bazoum mwezi uliopita.

Ecowas imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger
Ecowas imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger REUTERS - FRANCIS KOKOROKO

Waaandamanaji hao wakiwa wanapeperusha bendera ya nchi yao, ile ya Urusi, China na India, walisikika wakiishtumu nchi ya Ufaransa iliyokuwa Koloni yake na kulaani vikwazo vya kiuchumi vilivyowekewa nchi yake na Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

Aidha, waandamanaji hao walisikika wakisema hawaungi mkono mpango wa nchi za ECOWAS kuivamia nchi yao, ili kumrejesha rais Bazoum madarakani.

Baadhi ya raia nchini humo wameandamana kuunga mkono utawala wa kijeshi
Baadhi ya raia nchini humo wameandamana kuunga mkono utawala wa kijeshi REUTERS - STRINGER

Taarifa zinasema licha ya maandamano hayo, kuna baahi ya raia nchini humo ambao hawauungi mkono utawala wa kijeshi japokuwa wanaogopa kutoa msimamo wazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.