Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika umeifungia nchi ya Niger

Nairobi – Umoja wa Afrika (AU) umeifungia nchi ya Niger kushirika katika shughuli zote zinazohusiana na muungano huo kutokana na mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.

Jeshi nchini Niger limesema litarejesha utawala wa kiraia baada ya miaka mitatu
Jeshi nchini Niger limesema litarejesha utawala wa kiraia baada ya miaka mitatu © Stringer / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kitengo cha amani na usamala katika umoja huo kimetoa wito kwa nchi wanachama wa AU kujiepusha na masuala yoyote yanayoweza kuunga mkono na kuidhinisha mapinduzi ya kijeshi na Niger.

Umoja huo pia umesisitiza wito wake kwa viongozi wa kijeshi nchini Niger, kumuachia huru rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Mohamed Bazoum.

Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi Ecowas, umetishia kutumia nguvu za kijeshi kumrejesha madarakani rais Bazoum.

Kwa upande wake jeshi la Niger limesema utawala wa kiraia utarejeshwa tu baada ya muda wa miaka mitano, mpango ambao umepingwa vikali na Ecowas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.