Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Burkina Faso: Muungano dhidi ya kutokujali kwa uhalifu unadai uchunguzi kuhusu mauaji ya Rollo

Nchini Burkina Faso, muungano wa mashirika dhidi ya kutokujali kwa uhalifu na unyanyapaa wa jamii kwa mara nyingine tena unapaza sauti kwa mauaji ya watu wapatao ishirini mnamo mwezi Machi 8, 2023, katika wilaya ya Rollo, katika jimbo la Centre-Nord.

Jeshi la Burkinabe likishika doria karibu na kambi ya kikosi cha wanajeshi wa RSP, Septemba 29, 2015.
Jeshi la Burkinabe likishika doria karibu na kambi ya kikosi cha wanajeshi wa RSP, Septemba 29, 2015. AFP PHOTO / SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Daouda Diallo, katibu wa Muungano dhidi ya kutokujali kwa uhalifu, magari kadhaa yakiwa na watu wenye silaha waliokuwa wamevalia sare sawa na wanajeshi wa Burkina Fso walivamia kijiji cha Toessin-Foulbè.

Baada ya kufanya upekuzi katika kijiji hicho, watu hawa wenye silaha waliondoka na watu wapatao ishirini ambao inadaiwa waliwaua. Mungano dhidi ya kutokujali kwa uhalifu na unyanyapaa wa jamii unadai uchunguzi huru na usio na upendeleo wa mahakama ili kila aliyehusika aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

'Huzuni na hasira'

"Ni kwa huzuni na hasira kwamba tumejifunza juu ya kile kilichotokea huko Rollo, hasa katika kijiji cha Toessin-Foulbè, ambacho kilivamiwa na watu wenye silaha kutoka Burkina Faso, wakiwa wamevalia sare za jeshi, wakiandamana na raia wengine wenye silaha, pia waliotambuliwa kwa jina la VDP [Volunteers for the Defence of the Homeland] waliowasili asubuhi ya Machi 8, baada ya saa tatu  asubuhi, kijijini hapo. "

"Waliwakusanya wenyeji wote na, baada ya kuwakusanya, waliwaondoa katika kundi wanaume wote ambao waliwaua mita chache eneo walikokuwa wamekusanywa. Wauaji  walitoa tamko la kutozika miili hiyo. "

'Kuharakisha uchunguzi'

"Baada ya kuangalia na kulinganisha vyanzo mbalimbali, tuliona ni muhimu kuiomba mamlaka ya Burkina Faso ili kuwe na uchunguzi wa haraka kwa tukio hili. Lengo ni kuwaambia raia kwamba vikosi vyetu vilio kwenye uwanja wa vita, vinavyopigana usiku na mchana, havipo kwa kuhatarisha usalama wa raia. Ndio maana inabidi upelelezi wa haraka ufanyike ili kubaini majukumu, kubaini wahusika ili kuwabaini watu hao na kudumisha na kutafuta kuimarisha imani kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyopigana usiku na mchana kudumosha usalama wa wananchi wa Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.