Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Angalau raia 12 wauawa katika shambulio kaskazini mwa Burkina Faso

Karibu raia kumi na wawili waliuawa Alhamisi katika shambulio linalodaiwa na wanajihadi kaskazini mwa Burkina Faso, shirika la habari la AFP limesema likinukuu vyanzo vya ndani siku ya Jumatatu.

Wanajeshi wa Burkina faso wakishika doria katika moja ya mitaa ya Ouagadougu.
Wanajeshi wa Burkina faso wakishika doria katika moja ya mitaa ya Ouagadougu. © Olympia de Maismont / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, "kkundi la magaidi" lilishambulia kijiji cha Aorema, kilicho karibu kilomita kumi kutoka Ouahigouya, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini, wakaazi wa eneo hilo wameelezea AFP.

"Washambuliaji walirusha risasi dhidi ya kundi cha vijana walioketi kwenye kioski (mgahawa usio rasmi). Vijana saba walifariki papo hapo na watu watatu walifariki dakika chache baada ya kufikishwa makwao. Watu wengine wawili, walijeruhiwa na risasi, lakini  walifariki kutoka na majeraha, "mmoja wao amesema.

Kulingana na mkaazi mwingine, idadi ni "wafu kumi na nne", na watu kadhaa waliojeruhiwa ambao walifariki kutokana na majeraha katika siku zilizofuata shambulio hilo. 

Shambulio hilo lilithibitishwa na chanzo cha usalama, kuhakikisha kuwa "shughuli zinaendelea" katika eneo hilo, bila kutoa idadi kamili ya watu walioouawa.

Baada ya shambulio hili, sheria ya kutotoka nje usiku ilitangazwa katika mkoa wote wa Kaskazini mwa Burkina Faso, kwenye mpaka wa Mali ambao unalengwa mara kwa mara na wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.