Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Watu 14 wameuawa baada ya kushambuliwa na wanajihadi

NAIROBI – Watu katu ya 12 na 14 wameuawa Kaskazini mwa Burkina Faso, katika eneo ambalo linaendelea kushuhudia mashambulio ya mara kwa mara na makundi ya kijihadi.

Watu wenye silaha wamendelea kutatiza usalama wa raia nchini Burkina Faso
Watu wenye silaha wamendelea kutatiza usalama wa raia nchini Burkina Faso © RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa kijiji cha Aorema, karibu na mji wa  Ouahigouya, kulikotokea shambulio hilo, wamesema mauaji hayo, yalitokea wiki iliyopita, huku agisa mmoja wa usalama akithibitisha lakini hakusema idadi ya watu waliouawa.

Imebainika kuwa watu waliokuwa na silaha, waliwavamia vijana waliokuwa mkahawani na kuanza kuwapiga risasi, saba wakipoteza maisha papo hapo.

Aidha, wakaazi wa kijiji hao wamesema, mauaji haya yamekuja baada ya wanajihadi hao kuwatahdharisha vijana kukutana katika mkahawa huo uliolengwa.

Shambulio hili limekuja baada ya uongozi wa jimbo la Kaskazini na maeneo jirani kutangaza makataa ya watu kutembea kati ya saa nne usiku mpaka saa 11 alfajiri, lengo likiwa ni kusaidia juhudi za kukabiliana na wanajihadi wa kiislamu.

Mwezi uliopita, wanajihadi hao waliwauwa wanajeshi 51 Kaskazini mwa nchi hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa mauaji katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.