Pata taarifa kuu

Makataa ya watu kutembea nje yatangazwa Burkina Faso

NAIROBI – Mamlaka nchini Burkina Faso, zimetangaza makataa ya watu kutembea       katika maeneo ya kaskazini na baadhi ya maeneo ya katikati mwa nchi, lengo likiwa ni kusaidia juhudi za kukabiliana na wanajihadi wa kiislamu.

Ibrahima Traoré, rais wa Burkina Faso
Ibrahima Traoré, rais wa Burkina Faso © Kilaye Bationo / AP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa wakati ambapo kwa kipindi kirefu sasa, mashambulio ya wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo, yamesababisha vifo vya maelfu ya raia, polisi na wanajeshi, huku zaidi ya watu milioni mbili wakilazimika kukimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa gavana wa eneo la kaskazini Kouilga Albert Zongo, makataa haya yataanza saa nne usiku saa za Burkina Faso hadi saa kumi na moja asubuhi, kuanzia Machi 3 hadi Ijumaa ya Machi 31.

Chini ya makataa haya, raia hawataruhusiwa kutembea usiku, wala kutumia vyombo vya usafiri vya magurudumu mawili au manne, hatua ambayo mamlaka zinasema italisaidia jeshi kudhibiti usalama kwenye eneo linalopakana na Mali, Ghana na Togo.

Haya yanajiri wakati huu ambapo juma moja lililopita, askari zaidi ya 50 waliuawa katika shambulio la kushtukiza lililotekelezwa na wanajihadi wa kiislamu ambao wameongeza mashambulio katika siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.