Pata taarifa kuu

Burkina: Watu 18 wauawa katika mashambulizi mawili ya watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi

Takriban raia 18, wakiwemo wasaidizi kumi na sita wa jeshi, waliuawa Alhamisi katika mashambulizi mawili ya watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Burkina Faso, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu vyanzo vya usalama leo Ijumaa.

Wanajeshi wa Burkina Faso wakito ulinzi kwenye moja ya barabara ya mjini Ouagadougou, Burkina Faso mnamo Oktoba 1, 2022.
Wanajeshi wa Burkina Faso wakito ulinzi kwenye moja ya barabara ya mjini Ouagadougou, Burkina Faso mnamo Oktoba 1, 2022. REUTERS - VINCENT BADO
Matangazo ya kibiashara

"Shambulio la kwanza lililenga ngome ya watu waliojitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi (VDP) huko Rakoegtenga", mji ulioko katika jimbo la Bam (kaskazini), amebaini afisa wa VDP.

Kulingana na chanzo hicho, " watu sita kutoka kikosi cha watu wanaojitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi waliangamia (waliuawa) katika mashambulizi hayo. Mwanamke mmoja pia aliangamia wakati wa shambulio hili, na hivyo kufikisha idadi ya vifo vya watu saba". "Pia kuliripotiwa majeruhi kadhaa, ambao baadhi yao wako katika, hali mbaya na wamesafirishwa hadi Ouagadougou kwa uangalizi zaidi," ameongeza afisa huyo wa VDP.

Afisa huyo anasema, shambulio la pili lilifanyika katika mkoa wa Nayala (kaskazini-magharibi) "mchana, wakati msafara uliosindikizwa na wajitolea na askari walianguka kwenye shambulio la kuvizia kwenye mhimili wa Siena-Saran ". Shambulio hilo liliua wasaidizi zaidi ya kumi na raia mmoja.

Vyanzo vya usalama vilivyohojiwa na shirika la habari la AFP vimethibitisha "mashambulizi haya mawili ya wanajihadi" bila kutoa tathmini sahihi, vikitaja tu "hasara kubwa kwa upande wa vikosi vya usalama".

Burkina Faso, hasa kaskazini, imekabiliwa tangu 2015 na kuongezeka kwa mashambulizi ya makundi ya wanajihadi yanayohusishwa na Al-Qaeda na Islamic State. Mashambulizi ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na takriban watu milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao. Wiki iliyopita, takriban wanawake 60 na watoto wachanga walitekwa nyara karibu na Arbinda kaskazini mwa Burkina, na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.