Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-ELIMU-USALAMA

Burkina Faso: Kiongozi wa kijeshi akutana na wanafunzi wa vyuo vikuu

Kiongozi wa kijeshi nchini Burkinafaso Kapteni Ibrahim Traore amekutana jana Jumanne na wanafunzi wa vyuo vikuu kuwapa maelekezo na ushauri juu ya watu wanaokuza Ukabila na Udini katika mchakato wa kuwatafuta  vijana wanaopenda kujiunga na kikosi cha ulinzi wa taifa.

Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso
Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Swala la Usalama katika mikoa ya Wari na Waiguya ambako vyuo vikuu vimefungwa katika miji hiyo kutokana na usalama mdogo limeibuka katika mkutano huo ambapo kiongozi huyo amewahakikishia kuwa hivi karibuni vijana waliojiunga na jeshi watapelekwa huko baada ya kupewa mafunzo ya kijeshi.

“Wanapoona kwamba vita hivi tutashinda, swala ukabila limeanza na linajitokeza, msijiingize katika machafuko haya.”amesema Ibrahim Traore.

Kepteni Ibrahim Traore amezungumzia pia swala la ushirikiano wa kijeshi ambapo ameweka wazi kuwa hivi karibuni kutakuwa na marekebisho ya ushirikiano wa kijeshi na majeshi ya kigeni yalipo nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.