Pata taarifa kuu

Idadi ya wanawake waliotekwa nyara kaskazini mwa Burkina Faso yaweza kuongezeka hadi 80

Shahidi anayefanya kazi katika usalama wa eneo la Arbinda anafichua kwamba kwa kweli, vikundi vitatu vya wanawake vilitekwa nyara huko Boukouma, Wourougoudou na Trignaen, yaani sawa na wanawake 80 walitekwa nyara.

Arbinda, katika eneo la Sahel, mara kwa mara hulengwa na mashambulizi ya kigaidi.
Arbinda, katika eneo la Sahel, mara kwa mara hulengwa na mashambulizi ya kigaidi. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumapili, habari zimekuwa zikisambaa kuhusu utekaji nyara wa takriban wanawake hamsini, kutoka vikundi viwili, Alhamisi na Ijumaa, kitendo kilichotekelezwa na magaidi katika eneo la Arbinda, kaskazini mwa Burkina Faso. Taarifa hiyo imethibitishwa na mamlaka ya Burkina Faso katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumatatu asubuhi. Kwa kweli, sio vikundi viwili, lakini vitatu vya wanawake ambao walitekwa nyara katika maeneo matatu: Boukouma, Wourougoudou na Trignien. Ni sawa na takriban watu 80.

Mkazi huyu anayesaidia kutoa ulinzi wa eno la Arbinda anaeleza kuwa wanawake hao walikuwa wametoka kuchuma matunda wakati walipotekwa nyara. "Wakazi arobaini na watatu walichukuliwa kwa mara ya kwanza karibu na eneo la Boukouma. Kisha wengine 18 walitekwa nyara katika eneo la Wourougoudou, magharibi mwa Arbinda. Hatimaye, katika kijiji cha tatu, kinachoitwa Trignien, magaidi waliteka nyara kundi la mwisho la wanawake 16. Mmoja wao aliweza kutoroka. Katika ushuhuda wake, anaeleza kuwa wavamizi hao walichukua ng’ombe, kisha mateka hao walilazimika kuwapeleka wanyama porini, huku watekaji wakiwafuata kwa pikipiki. Walipofika Gnafo, magaidi hao walipumzika kwa ajili ya ibada ya swala. Hapo ndipo mwanamke huyo alipoweza kutoroka. Mwanamke wa pili aliyetekwa nyara alisema kuwa takriban watu kumi na watano walipelekwa katika eneo la Dala, ambapo wahalifu hao walichinja mbuzi, na kuwapa mchele wanawake waweze kupika. mwanamke huyo alitoroka wakati wa maandalizi ya chakula."

Gavana wa jimbo la Sahel amesema zoezi la kuwatafuta wanawake hao bado linaendelea. Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, raia wa Austria, alitoa wito wa "kuachiliwa mara moja na bila masharti" kwa mateka hao. Volker Türk alisema "ameshtushwa" na tukio hili ambalo, anasema, linaweza kuwa "shambulio la kwanza la aina yake kulenga wanawake kimakusudi" nchini Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.