Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina Faso: Wanawake 50 wametekwa na wanajihadi

Takriban wanawake hamsini walitekwa nyara kati ya Alhamisi na Ijumaa iliyopita, huko Arbinda, kaskazini mwa Burkina, eneo la Sahel.

Arbinda, dans la région du Sahel, est régulièrement ciblée par des attaques terroristes.
Arbinda, dans la région du Sahel, est régulièrement ciblée par des attaques terroristes. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo vya ndani, kundi la kwanza la wanawake arobaini walitekwa nyara siku ya Alhamisi na jingine la watu ishirini, siku iliyofuata, wengine walifaulu kukimbia na kisha kutoa taarifa hiyo.

Hakuna kundi lolote limekwisha dai kuhusuka na tukio hilo, lakini eneo hilo ni uwanja wa wanajihadi wa kundi la Jnim, Kundi lenye mafungamano na Al Qaeda.

Wakati mwingine eneo hilo hutaliwa na wanajihadi wa kundi linajojiita Islamic State tawi la ukanda wa Sahel.

Flore Berger, mtaalamu na mtafiti wa ukanda wa Sahel katika shirika la Global Initiative ((Mpango wa Dunia dhidi ya uhalifu wa kimataifa)

“Kumewahi kutokea utekekaji nyara kaskazini mwa Burkina Faso na katikati mwa Mali sio jipya, uzito ni tofauti kutokana na idadi ya wanawake wanaolazimika kwenda kutafuta matumizi mijini na hivyo kutekwa wakiwa njiani.”Ameeleza Flore Berger

Burkina Faso imekuwa ikitatizwa na makundi ya watu wenye silaha wanaowashambulia na kuwateka raia kwa muda sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.