Pata taarifa kuu

Ibrahim Traore: 'Magaidi' hushambulia zaidi raia

Rais wa mpito wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, amesema katika hotuba yake kwamba "awamu" mpya "imechochewa na magaidi", dhidi ya raia, siku chache baada ya wanawake karibu hamsini waliotekwa nyara na watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kijihadi kaskazini mwa nchi.

Arbinda iko katika eneo la Sahel, eneo ambalo limezingirwa na makundi ya wanajihadi, ambayo ni vigumu kuyasambaratisha.
Arbinda iko katika eneo la Sahel, eneo ambalo limezingirwa na makundi ya wanajihadi, ambayo ni vigumu kuyasambaratisha. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Leo awamu nyingine imechochewa na magaidi. Kwa upande wa kijeshi, wanajeshi wetu wamedhamiria kukabiliana nao, kwa hiyo wanaanza kushambulia raia wasio na hatia, kuwadhalilisha, kuwaua", ametangaza rais Traoré wakati wa mkutano huko Chuo Kikuu cha Ouagadougou na wanafunzi kutoka kote nchini.

Alhamisi na Ijumaa, takriban wanawake hamsini walitekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika maeneo mawili kaskazini na magharibi mwa mji wa Arbinda (kaskazini), kulingana na mamlaka ya eneo hilo. zoezi la kuwatafuta ardhini na angani unaendelea ili kuwapata. Umoja wa Mataifa ulitoa wito wa kuachiliwa "mara moja" kwa wanawake hao.

Arbinda iko katika eneo la Sahel, eneo ambalo limezingirwa na makundi ya wanajihadi, ambayo ni vigumu kuyasambaratisha. Kulingana na chanzo cha usalama kilichohojiwa na hirika la habari la AFP, "wakaazi wa Arbinda walianza kupewa msaada wa chakula kwa ndege siku ya Jumanne asubuhi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.