Pata taarifa kuu

Vita Tigray: Mwaka mmoja baada ya makubaliano ya Pretoria, amani iko mbali kufikiwa

Mwaka mmoja uliopita, Novemba 2, 2022, jeshi la Ethiopia na waasi wa TPLF wa Tigray walitia saini makubaliano ya amani mjini Pretoria, Afrika Kusini, ambayo yalimaliza miaka miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ethiopia. Kwa mujibu wa Umoja wa Afrika, takriban watu 600,000 waliuawa na wengine milioni moja kuyahama makazi yao. Mzozo huo umesababisha uharibifu mkubwa, na hali bado ni ya wasiwasi.

Mwakilishi wa serikali ya Ethiopia Redwan Hussein Rameto (kushoto) na mwakilishi wa TPLF Getachew Reda wakipeana mikono baada ya kutia saini makubaliano ya amani mjini Pretoria Novemba 2, 2022.
Mwakilishi wa serikali ya Ethiopia Redwan Hussein Rameto (kushoto) na mwakilishi wa TPLF Getachew Reda wakipeana mikono baada ya kutia saini makubaliano ya amani mjini Pretoria Novemba 2, 2022. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Mwaka mmoja baadaye, bunduki hazijakoma nchini Ethiopia. Huko Tigray, mapigano kati ya jeshi la Front for the Liberation of Tigray, TPLF, na lile la serikali ya shirikisho yamesitishwa, lakini wanamgambo wa Amarah, waliopewa jina la mkoa jirani unaokaliwa na moja ya watu wakubwa zaidi wa nchi, waendelea wanaendelea kupambana magharibi mwa nchi ambapo wanataka kupanua ushawishi wao. Washirika wa serikali ya Abiy Ahmed wakati wa vita, wanamgambo hawa wanabaini kwamba hawakujumuishwa katika makubaliano ya Pretoria na walikataa kuvunjwa kwao na kuingizwa katika jeshi la shirikisho pendekezo lililotolewa na Waziri Mkuu, kwa kuzingatia hii kama kudhoofika mbele ya vitisho kutoka kwa watu wengine, hasa Watigrayan. Kwa hivyo wanaendelea katika sehemu hii ya magharibi ya Tigray kile mtafiti huru René Lefort anaelezea kama "maangamizi ya kikabila".

"Kaskazini mwa Tigray, ni Waeritrea ambao wanaendelea kuwepo. Kama vile wanamgambo wa Amhara, jeshi la Eritrea lilishirikiana na serikali ya shirikisho wakati wa vita, lakini tena kutoelewana kuliibuka baada ya makubaliano ya Pretoria kati ya Rais wa Eritrea Issayas Afewerki na Waziri Mkuu wa Ethiopia. Eritrea inabaini kwamba serikali ya shirikisho haijafika mbali vya kutosha katika ukandamizaji na inataka kuondolewa kwa TPLF, anasema mtafiti huyo. Kwa hiyo inaendelea kuchukua kaskazini na sehemu ya mashariki ya Tigray. Kwa hivyo, kwa sehemu kubwa ya jimbo la Tigray, tuna uwepo wa wahusika wawili wakuu katika vita katika ukiukaji wa wazi wa mikataba ya Pretoria ambayo hata hivyo ilitoa nafasi ya kuondoka kwa vikosi hivi viwili: wanamgambo wa Amhara na vikosi vya Eritrea. »

Vurugu hizo zimeenea katika mikoa mingine

Ni kuendelea kwa vita huko Tigray. Huko Amhara, eneo lililo kusini mwa Tigray, wanamgambo wa Amhara waliasi serikali kuu. Mwezi Agosti, serikali ya Addis Ababa ilitangaza hali ya hatari kwa muda wa miezi sita kwa lengo la kutekeleza operesheni za kijeshi ili kurejesha udhibiti wa miji na hasa maeneo ya mashambani chini ya himaya ya wanamgambo wa Amhara.

Huko Oromia, ni Jeshi la Ukombozi la Oromia ambalo hivi majuzi limechukua silaha na linajaribu kuongeza ushawishi wake katika eneo hilo. Watu wa Amhara na Oromo ni watu wa kale wa Ethiopia ambao wametumia mamlaka mfululizo kwa karne nyingi; kwa upande wa mtafiti huru René Lefort, anasema kinachotokea leo si kingine ila "kurejeshwa kwa vita vya kutawala nchi", kutokana na mzozo wa hivi majuzi huko Tigray.

Raia wakiwa mstari wa mbele

Mzozo wa Tigray ulikuwa umewakosesha makazi zaidi ya watu milioni 4, milioni moja huko Tigray pekee, milioni nyingine katika mkoa wa Amhara. Mara nyingi wamewekwa kambiini, wengi wao hawajaweza kurudi nyumbani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, wengi wako katika dharura ya kibinadamu kutokana na ukosefu wa misaada ya kimataifa, lakini pia uharibifu wa karibu kabisa wa miundombinu. Huko Tigray, waangalizi wanakadiria kuwa zaidi ya 80% ya sekta za kilimo, viwanda, biashara na hospitali hazitumiki.

Kwa hiyo umaskini na magonjwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ya wakimbizi kutoka Tigray ambao, kwa wengi, wana alama katika miili yao na kiwewe cha vita: mauaji ya kiholela, mateso, ubakaji ... Uhalifu mwingi wa kivita ulifanyika katika miaka hii miwili, lakini mnamo Oktoba 4, mamlaka ya Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu nchini Ethiopia, chombo kinachohusika na kuchunguza mzozo huo, haikuongezwa muda, na hivyo kuzua hofu ya kutokuadhibiwa kabisa kwa uhalifu huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.