Pata taarifa kuu

Ethiopia : HRW yaitaka serikali kuhakikisha haki inapatikana kwa wahanga wa vita huko Tigray

Nairobi – Mwaka mmoja baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa amani uliomaliza vita vya miaka miwili kati ya wanajeshi wa serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa jimbo la Tigray, mashirika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Human Rights Watch, yameutaka umoja wa Mataifa na jumuiya ya Kimataifa, kuongeza shinikizo la kibinadamu kwa Serikali ya Ethiopia kuhakikisha haki inapatikana kwa wahanga wa vitendo vya ukatili, baada ya vita hivyo.

Shirika hilo limesema vikosi vya Eritrea, vilitekeleza mauaji, unyanyasaji wa kingono, utekaji nyara na uporaji
Shirika hilo limesema vikosi vya Eritrea, vilitekeleza mauaji, unyanyasaji wa kingono, utekaji nyara na uporaji AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Naibu mkurugenzi wa shirika hilo barani Africa, Laetitia Bader, amesema wakati serikali ya Ethiopia na washirika wake wa kimataifa wanapongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mwaka uliopita, raia katika maeneo yenye migogoro bado wanabeba mzigo mkubwa wa ukatili.

Bader amesema nchi inashuhudia wakatili wakirudia vitendo vya zamani bila kuwajibishwa, na serikali zinazounga mkono mapatano ya Ethiopia haziwezi kumudu kuangalia kando wakati machafuko nchini Ethiopia yanaongezeka.

Shirika hilo limesema vikosi vya Eritrea, vilitekeleza mauaji, unyanyasaji wa kingono, utekaji nyara na uporaji, na kuzuia usaidizi wa kibinadamu, na kukwamisha kazi ya waangalizi wa AU.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.