Pata taarifa kuu

Ethiopia : Uchunguzi wa UN kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu kutamatika wiki ijayo

Uchunguzi wa umoja wa Mataifa kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ethiopia, utatamatika wiki ijayo licha ya wachunguzi kuonya hatari ya kuongezeka kwa vitendo hivyo kwenye taifa linaloshuhudia mzozo.

Tume ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Ethiopia iliundwa mwaka 2021 na iliongezewa muda wa mwaka mmoja mwaka jana
Tume ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Ethiopia iliundwa mwaka 2021 na iliongezewa muda wa mwaka mmoja mwaka jana AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo licha ya wasiwasi wa uchunguzi huo kusitishwa, nchi wanachama zinazo siku hadi Jumatano ya wiki ijayo kuja na rasimu ya mapendekezo kuhusu kuongeza muda.

Pamoja na ripoti ya wataalamu maalumu wa umoja huo, msemaji wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Pascal Sim, amesema jumuiya ya kimataifa haijaonesha nia kutaka kuongezwa muda wa uchunguzi.

Kwa majuma kadhaa sasa Ethiopia, imekuwa ikishinikiza nchi tume hiyo kuachana na uchunguzi unaoendelea, pamoja na ukweli kuwa nchi hiyo inashuhudia vurugu kwenye êneo la Tigray na Amhara.

Tume ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu Ethiopia iliundwa mwaka 2021 na iliongezewa muda wa mwaka mmoja mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.