Pata taarifa kuu

Nigeria: Watu 17 wafariki na zaidi ya sabini hawajulikani baada ya boti yao kuzama

Zaidi ya watu 70 wametoweka nchini Nigeria tangu Jumamosi, wakati boti iliyokuwa imebeba wafanyabiashara wa eneo hilo ilipozama kwenye mto kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, maafisa wa idara ya huduma za dharura wamesema. 

Boti kwenye mto katika jimbo la Taraba, ambapo ajali ya boti ilitokea.
Boti kwenye mto katika jimbo la Taraba, ambapo ajali ya boti ilitokea. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Boti iliyokuwa imebeba takriban watu 100 wakiwemo wafanyabiashara na watoto ilipinduka siku ya Jumamosi katika jimbo la Taraba wakati ikielekea sokoni katika kijiji cha Mayo Ranewa wilayani Karim Lamido. "Watu sabini na watatu hawajulikani waliko na miili 17 imeopolewa mtoni," Ladan Ayuba, mkuu wa idara ya huduma za Dharura ya eneo hilo nchini Nigeria (NEMA), ameliambia shirika la habari la AFP.

Boti zisizotunzwa vizuri na mara nyingi zilizojaa kupita kiasi

Usafiri wa mtoni umeendelezwa sana nchini Nigeria, ambapo ajali hutokea mara kwa mara, hasa wakati wa msimu wa mvua, kwenye njia za maji zisizodhibitiwa, na boti zisizotunzwa vizuri na mara nyingi zimejaa kupita kiasi. Mapema mwezi huu, watu 40 waliripotiwa kutoweka na kudhaniwa kuwa wamekufa baada ya boti iliyokuwa imebeba abiria 50 kupinduka katika jimbo la Kebbi kaskazini magharibi mwa Nigeria, kulingana na mamlaka za eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.