Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Karibu miili thelathini yatolewa mtoni, zaidi ya mia moja haijapatikana

Waokoaji wa Nigeria wametoa miili zaidi ya thelathini kutoka Mto Niger kaskazini magharibi mwa Nigeria, ambapo boti ilizama siku moja kabla, ikiwa na zaidi ya abiria 180, wengi wao wakiwa wametoweka na kudhaniwa kuwa walizama.

Watu wakitoa miili ya watu waliokufa maji huko Ngaski, Nigeria, baada ya boti kuzama.
Watu wakitoa miili ya watu waliokufa maji huko Ngaski, Nigeria, baada ya boti kuzama. - AFP
Matangazo ya kibiashara

Manusura na viongozi wa eneo hilo wanasema abiria 20 tu walipatikana wakiwa hai katika shughuli za uokoaji siku ya Jumatano, kwa hivyo idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuongezeka hadi 160.

"Miili mitano ilipatikana jana (Jumatano), na wengine 31 leo Alhamisi, zoezi linaendelea, miili zaidi inatarajiwa kupatikana," Abubakar Shehu, amesema afisa wa eneo hilo ambaye amekuwa akisimamia shughuli ya uojoaji tangu ukingo wa mto.

Wakati wa msimu wa mvua, ajali za boti kuzama hutokea mara kwa mara mito nchini Nigeria, ambapo baadhi ya boti hupakia kuita kiasi na nyingi zimezeheka. Kuzama kwa boti hiyo Jumatano, hata hivyo, ni moja ya tukio hatari zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.