Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Nigeria: Takriban watu wanne wafariki baada ya jengo kubwa kuporomoka mjini Lagos

Jengo kubwa lililokuwa likijengwa liliporomoka Jumatatu huko Lagos, mji mkuu wa kiuchumi wa Nigeria, na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine kujeruhiwa lakini idadi inaweza kuongezeka, makumi ya wafanyakazi bado wamekwama chini ya vifusi.

Karibu na kilima cha uchafu chenye urefu wa zaidi ya mita kumi kupanda juu, kunaonekana wafanyakazi, ambao wamejaa vumbi. Angalau watano kati yao wamesema zaidi ya watu 40 walikuwa wakifanya kazi katika jengo hilo lilipoporomoka.
Karibu na kilima cha uchafu chenye urefu wa zaidi ya mita kumi kupanda juu, kunaonekana wafanyakazi, ambao wamejaa vumbi. Angalau watano kati yao wamesema zaidi ya watu 40 walikuwa wakifanya kazi katika jengo hilo lilipoporomoka. PIUS UTOMI EKPEI AFP
Matangazo ya kibiashara

Jengo hili la ghorofa 21 lililo kwenye mojawapo ya mitaa maridadi zaidi za Lagos, katika wilaya ya Ikoyi, liliporomoka kabla ya saa 3 usiku wakati wafanyakazi wengi walikuwa katika shughuli za ujenzi.

"Watu wanne ndio wanaripotiwa kuwa wamefariki kufikia sasa na watu wametwa wakiwa hai," amesema Ibrahim Farinloyer, wa idara a Usimamizi wa Dharura (Nema), ambaye amesema operesheni bado inaendelea.

Makumi ya watu wakwama

Karibu na kilima cha uchafu chenye urefu wa zaidi ya mita kumi kupanda juu, kunaonekana wafanyakazi, ambao wamejaa vumbi. Angalau watano kati yao wamesema zaidi ya watu 40 walikuwa wakifanya kazi katika jengo hilo lilipoporomoka.

Hapo awali, picha kutoka kwenye tovuti zilionesha umati wa watu karibu na kilima kikubwa cha uchafu. Ni nini kilisababisha kuanguka na ni watu wangapi wamenaswa chini ya vifusi bado haijulikani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.