Pata taarifa kuu

Mwanajeshi wa Kenya auawa katika shambulio nchini DRC

Mwanajeshi wa Kenya aliye katika kikosi cha jeshi la Afrika Mashariki mashariki mwa DRC ameuawa kufuatia shambulio la kuvizia na waasi wa M23.

Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) waliotumwa kama sehemu ya Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) wakiendesha gari huko Goma, mashariki mwa Kongo Jumatano, Novemba 16, 2022.
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) waliotumwa kama sehemu ya Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) wakiendesha gari huko Goma, mashariki mwa Kongo Jumatano, Novemba 16, 2022. AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya DRC Patrick Muyaya amesema kuwa mwanajeshi huyo alifariki siku ya Jumanne wakati wa mapigano kati ya wanajeshi wa eneo hilo na waasi wa M23 katika eneo la Kibumba.

Ni kifo cha kwanza kuripotiwa miongoni mwa wanajeshi wa Kenya tangu wajiunge na kikosi hicho mwaka jana.

Taarifa kutoka kwa jeshi la DRC ililaani mauaji hayo, na kuwalaumu M23.

Jeshi la DRC limesema shambulio hilo lililenga "kuzua mtafaruku" kati yake na EACRF.

Waasi wa M23 hawajatoa tamko lolote kuhusiana na shutuma hizo.

Mapigano yameanza tena hivi majuzi kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wanaojulikana kwa jina la Wazalendo katika maeneo ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Kikosi cha kikanda kimekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka DR Congo kwa kushindwa kukomesha ghasia.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema haitaidhinisha upya mamlaka ya EACRF, ambayo itakamilika mwezi Desemba.

Kenya imechangia zaidi ya wanajeshi 1,000 katika ujumbe huo ambao pia unajumuisha wanajeshi kutoka Uganda, Sudan Kusini na Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.