Pata taarifa kuu

Baraza la Usalama liko tayari kuamua juu ya kuondoka kwa MONUSCO DRC

Baraza la Usalama limekubali kwa makubaliano ya pande zote kuzingatia zoezi la kuondoa kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichotumwa nchini DRC, MONUSCO. Hivi karibuni rais wa DRC, na serikali ya Kinshasa, waliomba Umoja wa Mataifa mara kadhaa zoezi la kuondoa vikosi vya kulinda amani liidhinishwe na likubaliwe. Kwa hiyo Baraza limewajibu hivi punde Jumatatu usiku Oktoba 16 kwa tamko ambalo limezindua kuondoka kwa MONUSCO.

Wanajeshi wa MONUSCO wakipiga doria hukoKitshanga, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 11 Desemba 2022.
Wanajeshi wa MONUSCO wakipiga doria hukoKitshanga, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 11 Desemba 2022. © AFP - Guerchom Ndebo
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Huu ni ujumbe ambao rais Félix Tshisekedi na serikali ya Kongo wamekuwa wakisubiri kwa wiki kadhaa. Siku ya Jumatatu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilienda mbali ya "kuzingatia" maombi ya Kinshasa. Katika tamko hili, Braza la usalama la Umoja wa Mataifa linazindua zoezi la kuwaondoa walinda amani wa MONUSCO kutoka DRC: linahimiza serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kuwasilisha mwezi ujao mpango wa "kuondoa vikosi vya MONUSCO hatua kwa hatua na kwa uratibu."

Punguzeni mivutano kati ya raia na MONUSCO

Baaza la usalama la Umoja wa Mataifa Pia limetoa wito kwa Kongo na Rwanda kuzidisha mazungumzo kwa ajili ya amani, linalaani uungwaji mkono wowote kwa kundi la waasi la M23, na linahimiza kufanyika kwa uchaguzi kwa mafanikio mwaka 2023. Balozi wa Kongo katika Umoja wa Mataifa amekaribisha msimamo huu ambao unapaswa kusaidia kupunguza mvutano kati ya wakazi wa eneo hilo na MONUSCO.

Ni vigumu kujua kama kuondoka huku kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa kwa kulazimishwa katika miezi ya hivi karibuni na nchi wenyeji kama vile Mali, Sudan na Niger - au hata suala la walinda amani wanane waliokamatwa kwa kudumisha mfumo wa ukahaba karibu na kambi yao kumefanya Baraza la usalamala Umoja wa Mataifa kuchukuwa uamuzi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.