Pata taarifa kuu

DRC: Rais Tshisekedi anataka mpango wa kuondoa MONUSCO kuharakishwa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi akitoa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametaka kuharakishwa kwa mchakato wa kukiondoa nchini mwake kikosi cha kulinda amani MONUSCO ambacho kimekuwa nchini hiyo kwa miaka zaidi ya 20.

Tshisekedi amesema wakati umefika wa DRC kuchukua udhibiti wa nchi yake, huku akikishtumu kikosi hicho kwa kushindwa kumaliza utovu wa usalama, Mashariki mwa nchi yake
Tshisekedi amesema wakati umefika wa DRC kuchukua udhibiti wa nchi yake, huku akikishtumu kikosi hicho kwa kushindwa kumaliza utovu wa usalama, Mashariki mwa nchi yake REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi amesema wakati umefika wa DRC kuchukua udhibiti wa nchi yake, huku akikishtumu kikosi hicho kwa kushindwa kumaliza utovu wa usalama, Mashariki mwa nchi yake.

Felix Tshisekedi anawatuhumu MONUSCO kwa kushindwa kupambana na makundi ya waasi
Felix Tshisekedi anawatuhumu MONUSCO kwa kushindwa kupambana na makundi ya waasi REUTERS - EDUARDO MUNOZ

Kiongozi huyo amesema ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa umekosa kurejesha amani mashariki ya taifa lake licha ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka 25.

“Sio haki na haikubaliki watu wanaotajawa kuhusika na uhalifu mkubwa uliotajwa katika ripoti mbalimbali za wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya usalama nchini DRC wamesalia bila kuadhibiwa.” alisema rais Tshisekedi.

Monusco  ina wanajeshi zaidi ya elfu kumi na sita nchini DRC na ni ya pili katika ukubwa duniani.

Baadhi ya raia wa Goma Mashariki ya DRC awali waliandamana kutaka kikosi hicho kuondolewa nchini humo
Baadhi ya raia wa Goma Mashariki ya DRC awali waliandamana kutaka kikosi hicho kuondolewa nchini humo AFP - MICHEL LUNANGA

Walinda amani hao wamekuwa wakituhumiwa hata na raia wa taifa hilo kwa kile wanachodai ni kufeli katika majukumu yao, baadhi ya raia wakionekana kuaandamana wakiwataka waondoke kwenye taifa hilo.

Makundi ya waasi yameendelea kutekeleza mashambulio dhidi ya raia katika baadhi ya maeneo ya mashariki ya DRC hali ambayo imepelekea kutumwa kwa wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kusaidia katika urejeshwaji wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.