Pata taarifa kuu
USALAMA-MIUNDOMBINU

Bukavu: Takriban watu 10 wafariki kufuatia kuporomoka kwa shule

Takriban watu kumi waliuawa Alhamisi Agosti 10 huko Bukavu, kufuatia kuporomoka kwa jengo lililokuwa na shule ya kibinafsi. Kulingana na mashahidi, mkasa huo ulitokea saa sita mchana katika wilaya ya Bagira.

Mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, wa Bukavu, DRC.
Mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, wa Bukavu, DRC. Wikimedia/EMMANRMS
Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wanabaini kwamba maafisa waliokuwa kwenye mkutano walishangazwa na kuporomoka kwa jengo hilo la ghorofa nyingi.

“Ndiyo ni kweli, tayari nilituma gari la wagonjwa pale. Tayari tumetoa maiti nne, lakini kwa kweli tuko katika shida kubwa. Nimekosa kreni, kwa sababu, niliambiwa kuna watu ambao wamekwama chini ya lango ambalo lina uzito mkubwa, na kwamba hakuna mtu anayeweza kuliinua isipokuwa kreni, "alisema Meya wa Bagira, Patience Bengehya Wangwabo Alhamisi jioni kulingana na Radio Okapi.

Amesema kutofuata viwango vya ujenzi ndio chanzo cha janga hili:

"Kwa kweli, chanzo cha mkasa huu ni ujenzi usio sahihi. Walikuwa katika ujenzi, hivyo jengo likaporomoka. Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika wilaya hiyo na watu wengine wengi walikuwa ndani jengo hili. Tayari tumeshatoa miili minne, pia kuna majeruhi ambao wamepelekwa hospitalini. Zoezi la kutafuta miili na watu ambao inawezka bado wako hai linaendelea, lakini kwa mikono ni kazi ngumu, tunahitaji kreni".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.