Pata taarifa kuu

Roma na Paris zaendelea na zoezi la haraka kuwaondoa raia wa kigeni nchini Niger

Ndege tatu tayari zimetua Paris na Rome ili kuwahamisha mamia ya raia wa Ufaransa, Italia na raia wengine kutoka nchi za kigeni, huku Ufaransa ikitarajia kumaliza zoezi hilo leo Jumatano, kufuatia mapinduzi ya kijeshi wiki iliyopita katika nchi hiyo ya kimkakati ya Afrika Magharibi.

Raia wa Ufaransa na raia wengine wa Ulaya ambao wamehamishwa kutoka Niger, siku chache baada ya jeshi lkunyakua mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Agosti 2, 2023.
Raia wa Ufaransa na raia wengine wa Ulaya ambao wamehamishwa kutoka Niger, siku chache baada ya jeshi lkunyakua mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Agosti 2, 2023. © STEPHANIE LECOCQ / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia hali inayojiri kwa sasa nchini Niger, ECOWAS ilitangaza Jumanne jioni kwamba wakuu wa majeshii wa nchi zinazounda jumuiya hiyo watakutana kuanzia Jumatano hadi Ijumaa mjini Abuja. Ujumbe wa ECOWAS, unaoongozwa na Mnigeria Abdulsalami Abubakar, unatarajiwa nchini Niger siku ya Jumatano, afisa mkuu wa jumuiya hiyo ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi na afisa wa kijeshi kutoka Niger wamesema kwa sharti la kutotajwa majina.

ECOWAS, inayoongozwa na rais wa Nigeria, Bola Tinubu, imewapa viongozi wa mapinduzi nchini Niger wiki moja hadi Jumapili ijayo, bila kutenga uwezekano wa matumizi ya nguvu ikiwa ni lazima, kumrejesha kwenye wadhifa wake rais wa zamani Mohamed Bazoum, aliyepinduliwa Julai 26 na wanajeshi wa kikosi cha walinzi wake wa urais.

Wakati huo huo, raia mia moja wa kigeni wanaoishi Niger wamewasili Roma Jumatano asubuhi, na walihamishwa na Italia. Kulingana na shirika la Ansa, Waitaliano 36 na Wamarekani 21 ni miongoni mwa raia waliohamishwa. Raia wa Italia karibu 500 walikuwa wanaishi Niger, wengi wao wakiwa wanajeshi.

Kwa upande wa Ufaransa, ambayo ina takriban raia 1,200 waliosajiliwa nchini Niger, "ndege mbili zilitua jana usiku. Ya pili saa kumi alfajiri . Ndege nyingine mbili zimesafii kwenda Niger, huku moja ikiropotiwa kutua (Niamey). ) na iingine bado inasafiri," mkuu wa jeshi la Ufaransa ameliambia shirika la habari la AFP mapema asubuhi.

Ndege ya pili itasafirisha kundi lingine la Wafaransa, Wanigeria, Wajerumani, Wabelgiji, Wacanada, Wamarekani, Waaustria na Wahindi, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa.

Huu ni uhamishaji wa kwanza mkubwa ulioandaliwa na Paris katika Sahel ambapo mapinduzi yameongezeka tangu 2020. Paris inataja uhamishaji huo na "vurugu zilizotokea" dhidi ya ubalozi wake siku ya Jumapili wakati wa maandamano ya chuki dhidi ya Ufaransa, na kwa "kufungwa kwa anga ambayo inawaacha wenzetu bila uwezekano wa kuondoka nchini kwa njia zao wenyewe".

Niamey, kupitia sauti ya mmoja wa viongozi wa mapinduzi, hata hivyo alitangaza usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano kufunguliwa tena kwa "mipaka ya ardhini na angani" ya Niger na nchi tano jirani (Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.