Pata taarifa kuu

Wakuu wa majeshi kutoka nchi za ECOWAS kujadili mapinduzi ya Niger

Nairobi – Maofisa wa ulinzi kutoka katika Jumuiya ya Ecowas, wanatarajiwa kukutana leo Jumatano mjini Abuja nchini Nigeria kujadili mapinduzi ya kijeshi yaliotokea nchini Niger wiki iliyopita.

Utawala wa kijeshi umetangaza kufunguliwa tena kwa mipaka yake na mataifa ya Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad
Utawala wa kijeshi umetangaza kufunguliwa tena kwa mipaka yake na mataifa ya Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad © AFP
Matangazo ya kibiashara

Awali Ecowas ilikuwa imewapa wanajeshi waliohusika na mapinduzi hayo kipindi cha wiki moja kurejesha utawala wa rais Mohamed Bazoum na kutishia kutumia nguvu iwapo hilo halitazingatiwa.

Tayari nchi ya umoja na ulaya ikiwemo Ufaransa zimeanza kuwaondoa raia wake nchini Niger, Paris ikiwasafirisha raia wake 250 kwa kutumia ndege tatu.

Nchi za EU zimeanza kuwaondoa raia wake
Nchi za EU zimeanza kuwaondoa raia wake © STEPHANIE LECOCQ / REUTERS

Hatua ya kuwaondoa raia hayo wa kigeni ikija kufuatia hatua ya waandamanaji kuvamia ubalozi wa Ufaransa siku ya Jumapili.

Italia nayo pia ikiwa imechukua hatua kama ya Ufaransa na nchi zengine za EU, Marekani nayo pia ikiwa imewaondoa raia wake.

Utawala wa kijeshi umetangaza kufunguliwa tena kwa mipaka yake na mataifa ya Algeria, Burkina Faso, Libya, Mali na Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.