Pata taarifa kuu

Burkina Faso, Mali na Guinea waonya dhidi ya uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Niger

Burkina Faso, Mali na Guinea, mataifa matatu yanayotawaliwa na jeshi, yameonya kwamba yanapinga vikali uingiliaji kati wa kijeshi nchini Niger ili kumrejesha Mohamed Bazoum, rais aliyetimuliwa mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi. 

Kanali Assimi Goïta, kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Mali (kushoto), na Kapteni Ibrahim Traoré, kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso.
Kanali Assimi Goïta, kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Mali (kushoto), na Kapteni Ibrahim Traoré, kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso. © Baba Ahmed/AP et Vincent Bado/Reuters - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Burkina Faso na Mali, katika taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari, zinathibitisha kwamba itachukuliwa "kama tangazo la vita" kwa nchi zao mbili.

Onyo hili linakuja siku moja baada ya tishio la matumizi ya "nguvu" yliyotolewa na viongozi wa Afrika Magharibi, wakiungwa mkono na washirika wao wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, mkoloni wa zamani katika eneo hilo, akishutumiwa na askari walionyakua mamlaka nchini Niger kwa kutaka "kuingilia kati kijeshi".

Soma pia

Niger: Utawala wa kijeshi washtumu Ufaransa kwa kuandaa uingiliaji kati wa kijeshi

Katika taarifa ya pamoja, serikali za Burkina Faso na Mali "zinaonya kwamba uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya Niger utazingatiwa kuwa tangazo la vita dhidi ya Burkina Faso na Mali".

Wanaonya kwamba uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya Niger utapelekea Burkina Faso na Mali kujitoa katika ECOWAS (Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi), pamoja na kupitishwa kwa hatua za kujilinda ili kusaidia vikosi vya jeshi na raia wa Niger".

Nchi hizi zinaongeza kwamba "wanakataa kutekeleza" vikwazo "haramu, haramu na kinyama dhidi ya raia na mamlaka ya Niger" vilivyochukuliwa huko Abuja.

Siku ya Jumapili, viongozi wa ECOWAS waliweka makataa ya wiki moja kwa utawala wa kijeshi nchini Niger kwa "kurejeshwa kamili kwa utaratibu wa kikatiba", wakisema "watatumia nguvu" ikiwa ni lazima.

Pia waliamua "kusimamisha miamala yote ya kibiashara na kifedha" kati ya nchi wanachama wake na Niger, na kufungia mali za maafisa wa kijeshi waliohusika katika mapinduzi hayo.

Katika taarifa tofauti, Guinea, ambayo serikali yake pia iliibuka kutoka kwa mapinduzi, "ilionyesha kutokubaliana kwake na vikwazo vilivyopendekezwa na ECOWAS, ikiwa ni pamoja na kuingilia kijeshi" na "iliamua kutotumia vikwazo hivi ambavyo inaviona kuwa haramu na vya kinyama". Conakry "inaitaka ECOWAS kufikiria upya msimamo wake".

Shinikizo la kushinikiza wahusika wa mapinduzi ya Julai 26 kurejesha haraka "utaratibu wa kikatiba" linaongezeka, kutoka kwa washirika wote wa Magharibi na Afrika huko Niger, nchi ambayo inachukuliwa kuwa muhimu katika vita dhidi ya makundi ya wanajihadi kwa miaka kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.