Pata taarifa kuu

Niger: ECOWAS yataka jeshi kurejesha utawala wa kiraia

Viongozi wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magahribi ECOWAS waliokutana jijini Abuja, wamelipa jeshi nchini Niger muda wa wiki moja kuachia madaraka na kuruhsu kurejeshwa kwa serikali ya rais Mohamed Bazoum iliochaguliwa kikatiba.

Aidha viongozi wa ECOWAS wametishia kutumia nguvu iwapo jeshi halitatii wito huo
Aidha viongozi wa ECOWAS wametishia kutumia nguvu iwapo jeshi halitatii wito huo REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao aidha wametishia kutumia nguvu iwapo jeshi halitatii wito huo. Bola Tinubu, ni rais wa Nigeria na mwenyekiti wa ECOWAS.

“Ni lazima tuchukue hatua kali ilikumlinda rais Bazoum, kuvurugwa kwa utaratibu kwa kidemokrasia kumewafanya raia wa Niger kuwa katika sintofahamu na mazingira magumu.” alisema rais Bola Tinubu.

00:27

Rais Bola Tinubu kuhusu Niger

Aidha rais Tinubu ameeleza Jumuiya hiyo inahitaji kuwepo na nguvu na uthabiti kuhusu hali ya Bazoum pamoja na uhuru na kurejeshwa kwa serikali iliyochaguliwa kikatiba.

Katika hatua nyingine, viongozi wa kijeshi nchini Niger wameionya ECOWAS dhidi ya uingiliaji wowote wa kijeshi katika masuala ya nchi hiyo.

Licha ya shinikizo za viongozi wa ECOWAS, Jumuiya hiyo imetangaza vikwazo dhidi ya Niger, kwa kutangaza kufungwa kwa mipaka kati ya nchi hiyo na nchi jirani, lakini pia kuzuia safari za angaa.

Akizungumza na mwandishi wa RFI Claire Fages, Waziri Mkuu wa Niger Mahamadou Ouhoumoudou amekuwa na kauli hii.

“Niger ni nchi ambayo haina baharí kwa hivyo mipaka ya ardhini na angani inapofungwa wanachi ndio wanaohangaika sana lakini pia vikwazo vya fehda kwa nchi hii isiyokuwa na uchumi imara, hali hii inakuwa mbaya zaidi.” alieleza Mahamadou Ouhoumoudou.

00:43

Waziri Mkuu wa Niger Mahamadou Ouhoumoudou

Vikwazo vya ECOWAS vinakuja baada ya Umoja wa Ulaya Jumamosi iliyopita, kutangaza kusitisha msaada wa kifedha na ushirikiano wa kiusalama na Niger, baada ya jeshi kuchukua madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.