Pata taarifa kuu

Mapinduzi nchini Niger: Algeria "yaonya" ECOWAS dhidi ya uingiliaji wowote wa kijeshi

Hali nchini Niger inaendelea kutikisa kanda hiyo ndogo, na Algeria imejibu siku ya Jumanne Agosti 1 kwa maamuzi yaliyochukuliwa katika mkutano wa kilele wa ECOWAS siku ya Jumapili. Wakati taasisi hiyo ya Afrika Magharibi imetoa makataa ya wiki moja kwa viongozi wa mapinduzi nchini Niger kumrejesha Rais Mohamed Bazoum kwenye wadhifa wake, diplomasia ya Algeria inatoa "onyo" kwa hofu ya kuongezeka kwa mvutano katika kanda nzima.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf mnamo Juni 22, 2023 mjini Berlin.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf mnamo Juni 22, 2023 mjini Berlin. AP - Fabian Sommer
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria inazingatia ushiriki wa kijeshi uliokusudiwa na ECOWAS kama chaguo la "bahati mbaya". Bila kutaja hata kidogo jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, diplomasia "inaonya na kutoa wito wa tahadhari na kujizuia mbele ya nia ya kuingilia kijeshi kwa wanajeshi wa kigeni (...), hali ambayo ni mambo ya kutatiza na kuzorota kwa mgogoro wa sasa".

Serikali ya Algeria imebaini kwamba "kurejea kwa utaratibu wa kikatiba lazima kukamilishwe kwa njia za amani", ili kuepusha nchini Niger na eneo zima "ongezeko la ukosefu wa usalama na ukosefu wa utulivu".

Algeria ni mojawapo ya nchi zinazolaani mapinduzi hayo kuanzia saa zake za kwanza. Inachukua fursa ya taarifa hii mpya kwa vyombo vya habari "kuthibitisha tena kumuunga mkono rais halali wa Niger", Mohamed Bazoum.

Kauli hii inajiri wakati Ufaransa ikianza shughuli ya kuwahamisha raia wake siku ya Jumanne, na utawala wa kijeshi wa CNSP umelishutumu jeshi la Ufaransa kwa kutaka kuingilia kijeshi ili kumwachilia huru rais aliyeondolewa madarakani. Madai ambayo Paris imekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.