Ufaransa kuwaondoa raia wake nchini Niger
Nairobi – Ufaransa inatarajiwa kuaanza kuwaondoa raia wake kutoka Niger, ambapo mapinduzi ya wiki iliyopita yamesababisha maandamano ya kupinga Ufaransa, ubalozi wa Paris mjini Niamey umeeleza.
Imechapishwa:
Niger imekuwa nchi ya tatu katika ukanda wa Sahel katika kipindi cha chini ya miaka mitatu kushuhudia mapinduzi baada ya Mali na Burkina Faso.
Utawala wa Rais Mohamed Bazoum uliangsuhwa wiki iliyopita na wanajeshi maalum kutoka katika kikosi chake cha walinzi.
Watu wenye silaha wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya raia wa mataifa hayo hali ambayo imechangia kuyumba kwa uchumi wake, baadhi ya mataifa ya ukanda huo yakitajwa kuwa mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani.
Waandamanaji walionekana wakiwasha moto nje ya lango la ubalozi wa Ufaransa nchini Niger hali hii ikitajwa kuwa mojawapo ya Ufaransa kutangaza kuwaondoa raia wake.
Viongozi wa Afrika Magharibi, wakiungwa mkono na washirika wao wa Magharibi, walitishia kutumia nguvu kurejesha utawala wa rais Bazoum uliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kutangaza vikwazo vya kifedha kwa wanajeshi waliohusika na mapinduzi hayo.