Pata taarifa kuu

Niger: Maafisa wakamatwa, akiwemo Waziri wa Petroli na kiongozi wa chama cha PNDS

Nchini Niger, viongozi wa kisiasa wamekamatwa, akiwemo Waziri wa Mafuta, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo Mahamadou Issoufou, na kiongozi wa chama cha PNDS.

Waziri wa Madini wa Niger Hadiza Ousseini, hapa ilikuwa katika mji wa Niamey mnamo Mei 4, 2023, pia amekamatwa na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani.
Waziri wa Madini wa Niger Hadiza Ousseini, hapa ilikuwa katika mji wa Niamey mnamo Mei 4, 2023, pia amekamatwa na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani. © BOUREIMA HAMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetoka tu kuamua juu ya vikwazo dhidi ya serikali ya Niger, huko Niamey, maafisa wengine wa serikali ya Mohamed Bazoum wamekamatwa, kulingana na duru za kuaminika nchini Niger siku ya Jumatatu hii, Julai 31.

Baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani Hama Amadou Souley na Waziri wa Uchukuzi Oumarou Malam Alma, waliokamatwa katika masaa ya mapema ya mapinduzi, Waziri wa Mafuta Abba Sani Issoufou Mahamadou, mtoto wa rais wa zamani Issoufou Mahamadou, mpatanishi katika mgogoro wa sasa, na rais wa Chama cha PNDS-Tarayya, Foumakoye Gado, pia wamekamatwa.

Wawili hao, siku tatu zilizopita, walikamatwa wakiwa na wenzao waliojeruhiwa, katika hospitali, baada ya kisa cha moto kuripotiwa katika makao makuu ya chama chao. Waandamanaji wanaounga mkono viongozi wa mapinduzi kisha walichoma moto karibu magari hamsini. Saa sita mchana, pia Waziri wa Madini, Ousseini Hadizatou Yacouba, alikamatwa na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani.

Vyanzo vya karibu na chama pia havikuwa na taarifa yoyote kuhusu Waziri wa Fedha Ahmat Jidod na Abdou Rabiou, Waziri wa Mipango.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.