Pata taarifa kuu

Niger: Utawala wa kijeshi washtumu Ufaransa kwa kuandaa uingiliaji kati wa kijeshi

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, ambayo imesomwa na Kanali-Meja Amadou Abdramane, CNSP inatangaza kwamba "Ufaransa ilifanya mkutano katika makao makuu ya kikosi cha walinzi wa taifa ili kupata vibali muhimu vya kisiasa na kijeshi".

Picha hii ya skrini ya video kutoka ORTN - Télé Sahel mnamo Julai 31, 2023 inamuonyesha Kanali-Meja Amadou Abdramane akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa.
Picha hii ya skrini ya video kutoka ORTN - Télé Sahel mnamo Julai 31, 2023 inamuonyesha Kanali-Meja Amadou Abdramane akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa. © AFP -
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, ambayo imesomwa na Kanali-Meja Amadou Abdramane, CNSP inatangaza kwamba "Ufaransa ilifanya mkutano katika makao makuu ya kikosi cha walinzi wa taifa ili kupata vibali muhimu vya kisiasa na kijeshi".

Kulingana na viongozi a mapinduzi, idhini hizi zilitolewa na Waziri Mkuu wa muda Hassoumi Massaoudou na kamanda wa kikosi cha walinzi wa taifa, Kanali-Meja Midou Guirey.

Ili kuunga mkono kauli yake, CNSP inazungumzia hati zilizotiwa saini na mamlaka zilizoondolewa na kuidhinisha "mshirika wa Ufaransa kufanya mashambulizi ndani ya ikulu ya rais, ili kumwachilia Rais Mohamed Bazoum, aliyechukuliwa mateka".

Paris yakanusha

RFI haikuweza kuwasiliana na serikali ya zamani ya Niger au mamlaka ya Ufaransa ili kuthibitisha uhalisi wa hati hizi. Hata hivyo Mkuu wa diplomasia ya Ufaransa Catherine Colonna alikanusha siku ya Jumatatu mashtaka ya viongozi wa mapinduzi ambao wanashikilia mamlaka nchini Niger, ambayo Ufaransa ilitaka"kuingilia kati kijeshi" nchini humo. "Ni makosa," alisema kwenye kituo cha BFM. Pia Ufaransa iliona kuwa "inawezekana" kumrejesha rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohamed Bazoum kwenye wadhifa wake. "Na ni muhimu, kwa sababu uvunjifu wa amani huu ni hatari kwa Niger na majirani zake", ilibainisha.

Siku ya Ijumaa, CNSP pia ilishutumu "huduma za usalama za balozi za nchi za Magharibi" kwa "kurusha vitoa machozi na kutumia silaha zao" kwa waandamanaji na kusababisha majeruhi sita.

Ufaransa haijatajwa jina, lakini taarifa hiyo ilifuatia mkusanyiko wa watu waliojaribu kuingia kwenye lango la ubalozi siku ya Jumapili.

Kwa kujibu, diplomasia ya Ufaransa ilithibitisha kwamba "haina lengo lingine zaidi ya usalama wa raia wake", huku ikikumbusha kwamba inatambua tu mamlaka ya rais Bazoum na taasisi zilizochaguliwa kidemokrasia.

Vikwazo vya Ujerumani, Urusi yataka 'kuzuia'

Mwitikio mwingine wa kimataifa, katika ngazi ya kifedha wakati huu: baada ya Paris siku ya Jumamosi, Ujerumani ilitangaza kusitisha misaada yake ya maendeleo na msaada wake wa kibajeti kwa Niger. Hii inahusu malipo yote ya moja kwa moja na ushirikiano wote wa maendeleo wa nchi mbili. Berlin inasema iko tayari "kuchukua hatua zingine".

Umoja wa Ulaya uko kwenye mstari huo huo. Josep Borrell, mkuu wa diplomasia yaUmoja wa Ulaya, anasema kuwa EU itaunga mkono haraka na kwa uthabiti maamuzi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na hasa kizuizi cha kiuchumi kilichoamriwa mnamo Julai 30.

Kwa upande wake, Urusi inatoa wito kwa "wahusika wote kujizuia ili kuepusha watu kupoteza maisha". Msemaji wake ameeleza kuwa hali nchini Niger "inazua wasiwasi mkubwa" na kutoa wito "kurejeshwa kwa taasisi halali nchini humo haraka iwezekanavyo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.