Pata taarifa kuu

Mapinduzi nchini Niger: Ufaransa yasitisha misaada ya maendeleo na msaada wa bajeti

Wakati mapinduzi yaliyoongozwa na Jenerali Tchiani, ambaye anajidhihirisha kama kiongozi mpya wa Niger, yalichochea upinzani mkubwa kubwa kutoka jumuiya ya kimataifa, Ufaransa imetangaza Jumamosi kwamba inasitisha misaada yake ya maendeleo na uungaji mkono wa bajeti kwa Niger.

Niger, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, inategemea sana misaada kutoka nje. Ufaransa ilisitisha msaada kwa nchi hiyo siku ya Jumamosi ikitaka "kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba".
Niger, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, inategemea sana misaada kutoka nje. Ufaransa ilisitisha msaada kwa nchi hiyo siku ya Jumamosi ikitaka "kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba". AFP - -
Matangazo ya kibiashara

 

Ufaransa imesitisha "hatua zake zote za misaada ya maendeleo na bajeti" nchini Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais mteule Mohamed Bazoum, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imetangaza Jumamosi. Paris "inatoa wito wa kurejea bila kuchelewa kwa utaratibu wa kikatiba nchini Niger, na kumuachilia huru rais Bazoum, aliyechaguliwa na Waniger", inmebainisha wizara hiyo katika taarifa yake.

Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) limetoa euro milioni 97 mwaka wa 2021 katika nchi hii, miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani, kulingana na takwimu zinazopatikana kwenye tovuti ya AFD.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ziarani nchini Papua New Guinea, siku ya Ijumaa alilaani "kwa maneno makali mapinduzi ya kijeshi" nchini Niger, akisema kuwa ni "hatari" kwa eneo hilo, na kutoa wito "wa kuachiliwa" kwa Rais Bazoum.

Uungwaji mkono 'usiotetereka' kutoka Marekani

Kwa upande wake, Marekani inatoa uungwaji mkono wake "usiotetereka" kwa Rais Mohamed Bazoum. Haya ni maneno yaliyotumiwa jana na Anthony Blinken, mkuu wa diplomasia ya Marekani wakati wa mahojiano ya simu na rais wa Niger. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alitangaza, usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi hii, Julai 29, kwenye Twitter, kuwa amezungumza na Catherine Colonna, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa. "Tulijadili wasiwasi wetu wa pamoja juu ya matukio yanayotokea nchini Niger na haja ya haraka ya kuremjesha kwenye wadhifa wake rais Bazoum kama kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia," aliandika.

Wanajeshi elfu moja wa Marekani kwa sasa wametumwa nchini humo. Ufaransa ina wanajeshi 1,500. Wanajeshi hawa wa Ufaransa wanaendesha operesheni zao chini ya amri ya Niger kupigana dhidi ya makundi ya jihadi.

ECOWAS, kwa upande wake, imeitisha "mkutano maalum" kesho Jumapili Julai 30 huko Abuja. Umoja wa Afrika tayari umetoa kauli ya mwisho kwa waasi: Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linawapa wanajeshi waliiofanya mapinduzi siku 15 kurejesha "mamlaka ya kikatiba"

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.