Pata taarifa kuu

John Fru Ndi kuzikwa Jumamosi Kaskazini Magharibi mwa Cameroon

Mazishi ya John Fru Ndi yatafanyika Jumamosi Julai 29 katika eneo alikozaliwa, Kaskazini Magharibi mwa Cameroon. Mwanzilishi na kiongozi wa chama cha kihistoria cha upinzani cha Social Democratic Front (SDF), alikufa mnamo Juni 12 huko Yaoundé. Siku ya Ijumaa, mwili wake ulirudishwa Bamenda, ambapo mamia ya watu walikuwa wakiusubiri.

Raia wa Cameroon walikusanyika karibu na jeneza la John Fru Ndi kwenye uwanja wa michezo wa Palais des Sports huko Yaoundé mnamo Julai 27, 2023.
Raia wa Cameroon walikusanyika karibu na jeneza la John Fru Ndi kwenye uwanja wa michezo wa Palais des Sports huko Yaoundé mnamo Julai 27, 2023. AFP - DANIEL BELOUMOU OLOMO
Matangazo ya kibiashara

Mwili wa John Fru Ndi uliwasili katika jiji la Bamenda siku ya  Ijumaa, Julai 28, chini ya ulinzi mkali. Wanajeshi wa jeshi la taifa walisambazwa katika jiji lote na magari mengi ya kivita yalionekana. Waasi wanaotaka kujitenga kwa aeneo hilo linalozungumza Kiingereza walikuwa wametoa wito wa "kususia shughuli zote".

Mamia ya watu walikaidi marufuku ili kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi wa kihistoria wa upinzani ambaye alishawishi kizazi kizima, anaeleza Alexis Clamewe, afisa wa wchama cha SDF: "Kwanza, yeye ni kiongozi mwenye haiba. Ni mtu jasiri, mtu mwenye busara na mtu anayeipenda sana Cameroon. Ni mtu wa amani. Ni maneno kama hayo ambayo hunirudia ninapomfikiria mwenyekiti John Fru Ndi. Yeye ni mwongozo kwa vijana wote, kiongozi aliyeashiria kizazi kizima na ambaye ameingia katika kumbukumbu za cameroon. "

John Fru Ndi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 81, atazikwa Jumamosi katika kijiji alichozaliwa cha Baba II, karibu na Bamenda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.