Pata taarifa kuu

Cameroon: Watu kumi baada ya kuangukiwa na jengo katika mji wa Douala

Kuporomoka kwa jengo la makazi huko Douala, mji mkuu wa kiuchumi wa Cameroon, kumesababisha vifo vya watu kumi na wawili na watano kujeruhiwa vibaya, kulingana na awali ya afisa mkuu wa kikosi cha Zima moto, idadi iliyothibitishwa na diwani wa mji huo kwa shirika la habari la AFP siku ya Jumapili. 

Mnamo mwaka wa 2016, watu watano walifariki huko Douala baada ya kuangukiwa na jengo la ghorofa, na mamlaka ilitaja kuwa ajali hiyo ilisababishwa na suala la kutofuata viwango vya ujenzi. Mnamo mwezi Juni mwaka huo huo, mamlaka iliorodhesha majengo 500 yaliyojengwa bila kufuata viwango vya ujenzi.
Mnamo mwaka wa 2016, watu watano walifariki huko Douala baada ya kuangukiwa na jengo la ghorofa, na mamlaka ilitaja kuwa ajali hiyo ilisababishwa na suala la kutofuata viwango vya ujenzi. Mnamo mwezi Juni mwaka huo huo, mamlaka iliorodhesha majengo 500 yaliyojengwa bila kufuata viwango vya ujenzi. © Wikimedia Commons CC BY SA 4.0 J.NicolasKondaYansa
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, karibu saa saba usiku saa za Cameroon, jengo la ghorofa nne kaskazini mwa Douala liliporomoka kwenye jengo jingine la makazi la ghorofa moja, afisaa mkuu wa kikosi cha Zima moto ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina, na Charles Elie Zang Zang, diwani wa jiji la Douala amethibitisha tukio hilo.

Idadi ya waliofariki kufikia saa sita mchana ilikuwa watu kumi na wawili, 21 kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watano wakiwa katika "hali mbaya kabisa", kulingana na vyanzo hivi.

Hospitali ya Laquintinie huko Douala imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba ilipokea "watu kumi na tatu waliojeruhiwa vibaya katika mkasa huo", na kurekodi vifo viwili, ikiwa ni pamoja na "msichana wa miaka mitatu na msichana wa miaka 19".

Watu wengine kumi na mmoja waliolazwa ni watoto watatu wanaotunzwa katika chumba cha dharura cha watoto, vijana wawili, mwanamke wa miaka 28, na wanaume watano, uongozi wa hospitali umebainisha.

Mnamo mwaka wa 2016, watu watano walifariki huko Douala baada ya kuangukiwa na jengo la ghorofa, na mamlaka ilitaja kuwa ajali hiyo ilisababishwa na suala la kutofuata viwango vya ujenzi. Mnamo mwezi Juni mwaka huo huo, mamlaka iliorodhesha majengo 500 yaliyojengwa bila kufuata viwango vya ujenzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.