Pata taarifa kuu
USALAMA BARABARANI

Watu 16 wafariki katika ajali ya barabarani nchini Cameroon

Watu 15 walioandamana na mwili wa jamaa kwa mazishi yake walifariki siku ya Ijumaa nchini Cameroon katika mgongano kati ya basi lao dogo na lori ambalo dereva wake pia alifariki, Waziri wa Uchukuzi ametangaza hivi punde.

Mkasa huu mpya ulitokea siku 16 baada ya kifo cha abiria 15 wa basi ndogo lililobingirika mara mbili baada ya kupoteza njia mashariki mwa nchi. Ajali hiyo pia ilijeruhi watu 68.
Mkasa huu mpya ulitokea siku 16 baada ya kifo cha abiria 15 wa basi ndogo lililobingirika mara mbili baada ya kupoteza njia mashariki mwa nchi. Ajali hiyo pia ilijeruhi watu 68. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Barabara za nchi hii kubwa ya Afrika ya Kati mara kwa mara hukumbwa na ajali mbaya kwa sababu zinahusisha usafiri wa umma, hasa barabara ya National 3 (RN3) ambayo inaunganisha Yaoundé na mji mkuu wa kiuchumi wa Douala.

"Watu kumi na sita walifariki katika ajali hii, ikiwa ni pamoja na 15 ndani ya basi na mmoja katika lori", na watu watatu waliokuwa ndani ya basi dogo walinusurika lakini walijeruhiwa, Jean Ernest Masséna Ngallé Bibéhé, Waziri wa Uchukuzi ametangazwa kwenye redio ya serikali CRTV. Alikuwa anazungumza kutoka eneo la ajali, huko Edea, mji wa viwanda ulio kilomita 80 mashariki mwa Douala.

"Basi dogo lilikuwa limebeba mwili," ameongeza waziri bila kuweza kusema zaidi kuhusu sababu za kugongana kwa sura ya mbele kwa magari hayo mawili. CRTV imeripoti kuwa abiria hao walikuwa wazazi na ndugu wa marehemu waliokuwa wakienda kumzika.

RN3 ina mashimo na imepakana na tuta katika hali mbaya, lakini magari, hasa yale ya usafiri wa umma, mara nyingi yanajaa kupita kiasi, na huendeshwa kwa mwendo wa kasi, madereva wakati mwingine hupishana katika mazingira hatari.

Mkasa huu mpya ulitokea siku 16 baada ya kifo cha abiria 15 wa basi ndogo lililobingirika mara mbili baada ya kupoteza njia mashariki mwa nchi. Ajali hiyo pia ilijeruhi watu 68.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.