Pata taarifa kuu

DRC: Kwanini Felix Tshisekedi hatakwenda Ukraine na Urusi

Rais wa Kongo hatakuwa miongoni mwa viongozi wenzake wa Kiafrika katika mkutano wa kilele huko Saint Petersburg mnamo Julai 27 na 28. Ofisi ya rais ilitangaza siku ya Jumatatu Julai 24 kwamba "kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake, rais Tshisekedi kwa bahati mbaya hataweza kusafiri kwenda Ukraine na Urusi". Hakika, Mkuu wa Nchi alikuwa aende Kyiv kabla ya safari hii na alipaswa kukutana na Volodymyr Zelensky.

Félix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika zaiara yake huko Ndjamena mnamo Aprili 23, 2021.
Félix Tshisekedi, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), katika zaiara yake huko Ndjamena mnamo Aprili 23, 2021. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

"Ninawahakikishia, rais alikuwa na sababu madhubuti ya kusitisha safari yake," kinasema chanzo kilicho karibu na serikali ya DRC. Na mmoja wa wajumbe waliopo nchini Urusi anathibitisha: "Kwa Ukraine, kuhusu usalama wetu, hatujahakikishiwa, ni hatari sana. "Kwa kusafiri kwa treni kulizingatiwa kuwa ni safari ndefu sana, ngumu sana na haitawezesha kusafiri kwa muda mfupi, kimesema chanzo chetu.

Tatizo la wakati kwa hatua ya Urusi. Kwa upande wa ofisi ya rais, kwa wanataja wajibu kwa Félix Tshisekedi kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Francophonie 2023, mjini Kinshasa, Ijumaa hii, Julai 28. Zaidi ya yote, anaongeza mmoja wa wasaidizi wake, kwamba wakuu wa nchi wamethibitisha uwepo wao hivi karibuni.

Ofisi ya rais pia inahakikisha kwamba hakukuwa na shinikizo la kimataifa. "Marekani na Uingereza huenda ziliweza kutuma ujumbe  kusema kwamba halikuwa wazo zuri, lakini kwa kweli hoja hii" hana msingi wowote katika uamuzi huo, anasema mwanadiplomasia mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.