Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

ATMIS kuondoa wanajeshi wake wote nchini Somalia ifikapo mwishoni mwa mwaka

Kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, ambacho kilibadilishwa jina na kuwa ATMIS, kimekabidhi kambi tatu kwa jeshi la Somalia kama sehemu ya hatua ya kuanza kuwaondoa wanajeshi wote wa Umoja huo.

Kwa mujibu wa maazimio ya awali ya Baraza la Usalama, ATMIS ilianza kuwaondoa wanajeshi 2,000 siku chache zilizopita, mchakato unaopaswa kukamilika mwishoni mwa Juni.
Kwa mujibu wa maazimio ya awali ya Baraza la Usalama, ATMIS ilianza kuwaondoa wanajeshi 2,000 siku chache zilizopita, mchakato unaopaswa kukamilika mwishoni mwa Juni. © REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kikosi cha ATMIS, ambacho kilikuwa kimejumuisha zaidi ya askari 19,000 na maafisa wa polisi, kitalazimika kupunguzwa hadi sifuri mwishoni mwa 2024, na kuhamishwa taratibu kwa shughuli zake kwa vikosi vya Somalia. 

Shughuli hizi za kuondoa wanajeshi ni kwa mujibu wa ratiba ambayo Somalia na washirika wake wa kiulinzi na kiusalama wamekubaliana.

Wiki hii, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilirefusha muda wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, kwa miezi sita, huku ukijiandaa kuondoka kikamilifu kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Azimio la kuidhinisha ATMIS hadi mwisho wa 2023 lilipitishwa kwa kauli moja Jumanne, na kuweka kikomo kipya cha wanajeshi 14,626 kutoka Oktoba 1 hadi Desemba 31.

Kwa mujibu wa maazimio ya awali ya Baraza la Usalama, ATMIS ilianza kuwaondoa wanajeshi 2,000 siku chache zilizopita, mchakato unaopaswa kukamilika mwishoni mwa Juni. 

Somalia imeongoza juhudi za kuwapa mafunzo wanajeshi wake, wale wapya ambao wameingia katika jeshi la nchi. Na kuunda vikosi maalumu ya kupambana na uhalifu wa  Al Shabab. Kuna taarifa zinaeleza wanajeshi wao wanapokea mafunzo nchini Urusi, Ehiopia, na Uganda. Na wengine watapewa mafunzo maalumu ya kupambana na Al Shabab katika nchi za Kenya na Djibouti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.