Pata taarifa kuu
SOMALIA- USALAMA

Huenda Al Shabaab imeanza kujiimarisha, imeonya ATMIS

Wataalamu wa masuala ya usalama kwenye pembe ya Afrika, wameonya kuhusu uwezekano wa wapiganaji wa kiislamu wa Al Shabaab kujiimarisha, wakati huu wanamgambo hao wenye uhusiano na kundi la Al Qaeda, wakiongeza mashambulio.

Wapiganaji wa kundi la Al Shabab
Wapiganaji wa kundi la Al Shabab Feisal Omar/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa miezi kadhaa sasa baada ya kuwa kimya, kundi hilo limezidisha mashambulio kwenye mji mkuu Mogadishu na miji mingine, ambapo hadi sasa mamia ya watu wameuawa.

George Musamali, ni mtaalamu wa masuala ya usalama akiwa nchini Kenya.

“Serikali iliyoko nchini Somalia na ile iliyopita wamekuwa na ulegevu katika maswala ya usalama.” ameeleza George Musamali.

Mataifa yanayopakana na Somalia kama vile kenya, hutatizwa na mashambulio ya wapiganaji wa Al Shabaab katika maeneo yalioko mpaka na taifa hilo la Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.