Pata taarifa kuu

Somalia: Wanajeshi 54 wa Umoja wa Afrika waliuawa katika shambulio la Mei 26

Takriban wanajeshi 54 waliuawa katika shambulizi dhidi ya kambi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Uganda Mei 26 nchini Somalia, Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza huvi punde. "Tulirekodi hasara kubwa, maiti za wanajeshi 54 walioangamia, akiwemo mmoja wa makamanda wa kikoi hicho," Yoweri Museveni alisema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye akaunti yake rasmi ya Twitter Jumamosi jioni. 

Somalia inaendelea kuathirika kutokana na mizozo ya kisiasa isiyoisha.
Somalia inaendelea kuathirika kutokana na mizozo ya kisiasa isiyoisha. REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Waislam wenye itikadi kali wa Al Shabab, wenye mafungamano na Al-Qaeda walidai kuhusika na shambulio hilo huko Bulo Marer, kilomita 120 kusini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.

Ripoti ya kwanza ilitolewa baada ya shambulio la Mei 26 nchini Somalia. Takriban wanajeshi 54 waliuawa katika shambulio lililodaiwa na wanamgambo wenye itikadi kali wa Al-Shabaab dhidi ya kambi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AU) inayoshikiliwa na wanajeshi wa Uganda, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza kwenye Twitter Jumamosi jioni, ambaye aliongeza kuwa mmoja wa makamanda ni miongoni mwa wahanga.

Mashambulizi kwenye kituo cha Bulo Marer, kilichoko kilomita 120 kusini magharibi mwa Mogadishu, yalianza "karibu saa kumi na moja alfajiri" wakitumia gari ndogo iliyojaa vilipuzi na washambuliaji wa kujitoa mhanga, kamandi ya operesheni ya kudumisha amani nchini Somalia ATMIS imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. Shambulio lililothibitishwa na msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye.

"Mapigano kati ya magaidi na askari wa Atmis yalifuatia. Vikosi kutoka kitengo cha jeshi la anga la ATMIS na washirika walifanikiwa kuharibu silaha zilizokuwa zikimilikiwa na wanamgambo wa Al Shabab,” limeongeza shirika hilo, ambalo ni nadra kutoa ripoti kuhusiana na mashambulizi yanayolenga wanajeshi wake.

"Kulikuwa na mapigano makali. Vikosi vya AU na vikosi vya Somalia viliwatimua washambuliaji na hali ikarejea kuwa ya kawaida”, ameeleza kwa kina Mohamed Yerow Hassan, kamanda wa jeshi la Somalia, akithibitisha matumizi ya "gari lenye vilipuzi" .

Marekani "inalaani vikali" kitendo hiki, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller amesema katika taarifa yake. Nchi hiyo "inasimama pamoja na Somalia na Umoja wa Afrika katika vita vya kuushinda ugaidi na kuleta amani na utulivu kwa raia wa Somalia," ameongeza. Siku moja baada ya shambulio hilo, Washington ilidai kuharibu silaha na vifaa vilivyoibiwa na wanajihadi kutoka kwa kundi la Al-Shabab wakati wa shambulio la anga karibu na kambi ya kijeshi iliyoshambuliwa.

Al Shabab lajizatiti katika maeneo makubwa ya vijijini

Kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na Al-Qaeda, wamekuwa wakipigana kwa zaidi ya miaka kumi na tano dhidi ya serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, ili kuanzisha sheria ya Kiislamu nchini Somalia. Ili kukabiliana na uasi huu, AU ilituma mwaka 2007 kikosi kilichojumuisha askari 20,000, polisi na raia kutoka Uganda, Burundi, Djibouti, Ethiopia na Kenya, kiitwacho AMISOM. ATMIS ilichukua hatamu kutoka kwa AMISOM mnamo mwezi Aprili 2022, kwa lengo la kukabidhi jukumu kamili la usalama wa nchi kwa vikosi vya Somalia hadi mwisho wa mwaka 2024.

Wakifukuzwa nje ya miji mikubwa mwaka 2011-2012, Al Shabab wamesalia imara katika maeneo makubwa ya vijijini, ambapo wanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya usalama na malengo ya kiraia. Mnamo mwezi Mei 2022, walifanya shambulio kubwa kwenye kambi iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Burundi wa ATMIS kaskazini mwa Mogadishu. Mamlaka ya Somalia au AU haikutoa ripoti kuhusiana na shambulizi hilo, lakini vyanzo vya kijeshi vya Burundi viliripoti kuwa wanajeshi 45 waliuawa au kutoweka.

Rais wa Somalia Hassan, Sheikh Mohamoud, alitangaza "vita kamili" dhidi ya Al Shabab na kuanzisha mashambulizi ya kijeshi mwezi Septemba, yakiungwa mkono na ATMIS na mashambulizi ya anga ya Marekani. Operesheni hizi zilifanya iwezekane kuteka tena maeneo makubwa katikati mwa nchi. Mapema mwezi Januari, vikosi vya serikali viliuteka tena mji wa kimkakati wa Harardhere kama sehemu ya shambulio lililoanzishwa miezi mitano iliyopita, kwa msaada wa makundi ya raia wenye silaha.

Lakini Shebab wanaendelea kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kwa kulipiza kisasi. Mnamo Oktoba 29, 2022, mabomu mawili ya gari yalilipuka huko Mogadishu, na kuua watu 121 na kujeruhi 333, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea katika miaka mitano nchini humo.

Katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Februari, Katibu Mkuu Antonio Guterres alidai kuwa mwaka 2022 ulikuwa mwaka mbaya zaidi kwa raia nchini Somalia tangu 2017, hasa kutokana na mashambulizi ya Al-Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.