Pata taarifa kuu

UN yafanikiwa kuchangisha fedha za kukabili makali ya njaa kwenye pembe ya Afrika

NAIROBI – Umoja wa Mataifa na nchi wafadhili Jumatano ya wiki hii walifanikiwa kuchangisha kiasi cha dola za Marekani bilioni 2 na laki 4 kwa ajili ya kusaidia juhudi za kupunguza makali ya njaa kwenye nchi za Pembe ya Afrika, eneo ambalo linashuhudia ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40.

Idadi kubwa ya raia kwenye Pembe ya Afrika wanakabiliwa na athari za ukame na njaa
Idadi kubwa ya raia kwenye Pembe ya Afrika wanakabiliwa na athari za ukame na njaa AFP - MOHAMED ABDIWAHAB
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres, amesema watu zaidi ya milioni 32 kwenye mataifa ya Kenya, Somali na Ethiopia, wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kunusuru maisha yao.

Hata hivyo licha ya hatua hii, lengo la awali la kupata dola bilioni 7 halikufanikiwa, mashirika ya misaada yakitoa wito wa kupatikana kiasi hicho cha fedha kwa wakati.

"Mizozo juu ya mizozo inatishia maisha na ustawi wa mamilioni ya raia kwenye Pembe ya Afrika, ukame wa muda mrefu kuwahi kushuhudiwa, watu kukimbia baada ya miaka ya machafuko na utovu wa usalama, lazima tuchukue hatua sasa kuzuia mizozo kugeuka kuwa majanga."alisema Katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres.

00:40

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa UN kuhusu Pembe ya Afrika

Hatua hii inakuja wakati huu zaidi ya watu milioni moja nchini somali katika kipindi cha miezi minne wakiwa hawana malazi katika nchi yao wenyewe, kutokana na madhila kadhaa ikiwemo ukame, vurugu na mafuriko, imesema taarifa ya mashirika ya misaada ya kibinadamu.

Kulingana na shirika linalowashughulikia wakimbizi na baraza la wakimbizi la Norway, watu laki 4 na elfu 33, walilazimika kuhama nyumba zao kati ya Januari Mei 10, wakati ghasia za wanajihadi wa kiislamu zilipozuka katika eneo lililojitenga la Somalilanda.

Katika taarifa ya pamoja, mashirika hayo aidha yamesema, watu zaidi ya laki 4 na elfu 8 pia walihama makamzi yao kutokana na mafuriko yaliokumba vijiji mbalimbali huku watu wengine laki 3 na elfu 12 wakihama kutokana na ukame.

Taarifa yao imeongeza kuwa hadi sasa, idadi ya watu waliohama makazi yao nchini Somalia imefikia milioni 3.8, huku wengine milioni 6.7 wakikabiliwa na ugumu wa kupata chakula, wakati watoto zaidi ya nusu milioni wakikumbwa na utapiamlo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.