Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mauaji ya halaiki ya 1994: Rwanda yataka kukamatwa kwa watuhumiwa 55 nchini Malawi

"Serikali ya Rwanda imeomba usaidizi kutoka kwa serikali ya Malawi kubaini washukiwa 55 ambao kwa sasa wamejificha nchini Malawi. Watu hawa wanajulikana kama wababe wa kivita," Waziri wa Usalama wa Ndani wa Malawi, Ken Zikhale Ng'oma alisema, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Lilongwe.

"Washukiwa 55 kwa sasa wamejificha nchini Malawi. Watu hawa wanajulikana kama wababe wa kivita," kulingana na Wizara ya Usalama wa Ndani ya Malawi.
"Washukiwa 55 kwa sasa wamejificha nchini Malawi. Watu hawa wanajulikana kama wababe wa kivita," kulingana na Wizara ya Usalama wa Ndani ya Malawi. © SIMON WOHLFAHRT/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mauaji ya halaiki yaliua zaidi ya watu 800,000, kulingana na Umoja wa Mataifa, hasa Watutsi walioangamizwa kati ya mwezi Aprili na mwezi Julai 1994. Washukiwa hao 55 wanatafutwa kwa "vifo vya zaidi ya watu 2,000 katika baadhi ya makanisa", alisema Bw. Ng'oma, bila kutoa maelezo zaidi.

Ombi hili kutoka kwa Rwanda linakuja wiki chache baada ya kukamatwa nchini Afrika Kusini kwa Fulgence Kayishema, ambaye wakati huo alikuwa mmoja wa watu wanne wa mwisho wanaotafutwa na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kwa jukumu lao katika mauaji ya kimbari. Kayishema, ambaye alitumia lakabu nyingi na kughushi nyaraka, alisafiri kwa pasipoti ya Malawi.

Bw Ng'oma alisema mamlaka ilikuwa ikifanya "uchunguzi wa kina" kuelewa jinsi mtuhumiwa huyo, ambaye sasa ana umri wa miaka 62, alipata hati hiyo na hivi karibuni atatoa "ripoti kamili".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.