Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Alieu Kosiah, mbabe wa kivita wa zamani wa Liberia apatikana na hatia nchini Uswisi

Kwa mara ya kwanza nchini Uswisi, mshtakiwa amepatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu Alhamisi hii, Juni 1, 2023. Alieu Kosiah alikuwa afisa katika kundi la waasi la Ulimo wakati wa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia, kati ya mwaka 1989 na 1996. Alipigana dhidi ya  vikosi vya rais wa zamani Charles Taylor na alishutumiwa kwa kuamuru au kufanya mauaji ya watu 19, ubakaji mwingi, na hata kula moyo wa mtu.

Mahakama ya shirikisho ya jinai huko Bellinzona, Uswisi, Mei 5, 2016.
Mahakama ya shirikisho ya jinai huko Bellinzona, Uswisi, Mei 5, 2016. © Wikimedia Commons CC BY SA 4.0 NAC
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashirika yaliyoanzisha utaratibu huo dhidi ya Alieu Kosiah, mahakama imetoa uamuzi ambao haujawahi kushuhudiwa, hivyo kutuma ujumbe mzito duniani kote. Ukweli wa uhalifu wa kivita na miaka 20 jela iliyoamuliwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita imethibitishwa. Lakini wakati wa mchakato wa kukata rufaa, mahakama iliongeza uhalifu dhidi ya binadamu kwenye mashtaka. Uhalifu uliingia katika Kanuni ya Adhabu ya Uswisi mnamo mwaka 2011 pekee. Ukweli kwamba anatambuliwa kwa mara ya kwanza kwa makosa ya zamani ambayo ya miongo kadhaa hufanya kesi hili kuwa ya kihistoria.

Wito wa kuwafungulia mashitaka wahalifu pia nchini Liberia watolewa

Kwa mujibu wa Alain Werner, mkurugenzi wa shirika la Civitas Maxima, ambaye alitetea walalamikaji 4 kati ya 7, "Mahakama ya Uswisi inathibitisha kwamba inawezekana kushtaki uhalifu wa kimataifa nchini Uswisi, hata kwa vitendo vilivyofanywa umbali wa kilomita 7,000". Anaona kuwa uamuzi huu unatoa mfano ambao utawahimiza waathiriwa kutoa ushahidi na itaongeza shinikizo kwa wahalifu ambao bado wako huru.

Kwa kuzingatia kuwa makosa yalifanywa zamani na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha, upande wa mashtaka umejikita ushuhuda wa waathiriwa. Alieu Kosiah amekuwa akikanusha kila mara shutma dhidi yake. Kutoka Monrovia, Hassan Bility wa shirika lisilo la kiserikali la GJRP anasema serikali ya Liberia lazima ichukue hatua sasa na "kukomesha hali ya kutokujali" kabla haijachelewa. Hakika, hakuna mhalifu wa zamani wa Libeŕia ambaye amehukumiwa nchini humo tangu kumalizika kwa vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.