Pata taarifa kuu

Kifungo cha maisha jela: Kiongozi wa zamani wa waasi wa Liberia Kunti Kamara kukata rufaa

Aliyekuwa kamanda wa waasi Kunti Kamara atakata rufaa dhidi ya kifungo chake cha maisha jela kwa vitendo vya ukatili na kushiriki uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia (1989-1997), wakili wake ameliambia shirika la habari la AFP Alhamisi wiki hii.

Wakati wa vita vya kwanza kati ya viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia (1989-1997), Kunti Kamara alikuwa mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vuguvugu la Ukombozi wa Demokrasia (Ulimo), ambalo lilikuwa limechukua eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi na kuzuia wanamgambo wa Charles Taylor.
Wakati wa vita vya kwanza kati ya viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia (1989-1997), Kunti Kamara alikuwa mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vuguvugu la Ukombozi wa Demokrasia (Ulimo), ambalo lilikuwa limechukua eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi na kuzuia wanamgambo wa Charles Taylor. AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kesi isiyokuwa ya kawaida nchini Ufaransa, Mahakama ya Paris Jumatano jioni ilimhukumu mwanamgambo huyo wa zamani wa Liberia mwenye umri wa miaka 47 kifungo cha maisha jela kwa mfululizo wa unyanyasaji dhidi ya raia mwaka 1993-1994, ikiwa ni pamoja na mateso aliyofanyiwa mwalimu ambaye moyo wake ulidaiwa kuwa alikula, na kwa kutojali kwake mbele ya ubakaji wa mara kwa mara wa wasichana wawili matineja na askari waliowekwa chini ya mamlaka yake.

Kwa maneno yake ya mwisho mahakamani, mshtakiwa, mwenye upara na masharubu mengi, alipinga shutma dhidi yake Jumatano asubuhi. "Sina hatia leo, sina hatia kesho, nilikuwa askari wa kawaida tu," alisema Kunti Kamara.

"Uhalifu uliofanywa ni wa kutisha sana kuelezeka," alisema mbele ya majaji mwandishi wa habari na mwanaharakati wa Liberia John Stewart.

Wakati wa vita vya kwanza kati ya viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia (1989-1997), Kunti Kamara alikuwa mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vuguvugu la Ukombozi wa Demokrasia (Ulimo), ambalo lilikuwa limechukua eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi na kuzuia wanamgambo wa Charles Taylor. Ni katika eneo hili la Lofa ambapo "C.O Kundi" - kwa "afisa mkuu" - alishiriki katika mauaji dhidi ya raia ambao umemfanya afikishwe mahakamani huko Paris tangu Oktoba 10, kwa niaba ya mamlaka ya ulimwengu inayotekelezwa na Ufaransa kwa uhalifu mkubwa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.