Pata taarifa kuu

Liberia: George Weah awatimua washirika wake waliowekewa vikwazo na Marekani

Wananchi wengi nchini Liberia wamepigwa na mshangao mkubwa baada ya kusimamishwa kazi, Jumanne, Agosti 16, kwa maafisa watatu wakuu, wanaotuhumiwa kwa ufisadi katika ripoti ya hivi majuzi. 

Rais wa Liberia George Weah (hapa ilikuwa mwaka 2018) mnamo Jumanne, Agosti 16, aliwasimamisha kazi maafisa watatu wakuu walioshutumiwa na Marekani kwa ufisadi.
Rais wa Liberia George Weah (hapa ilikuwa mwaka 2018) mnamo Jumanne, Agosti 16, aliwasimamisha kazi maafisa watatu wakuu walioshutumiwa na Marekani kwa ufisadi. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Watu hao watatu, akiwemo mkurugenzi mkuu katika ofisi ya Rais George Weah, waliwekewa vikwazo na Marekani siku ya Jumatatu kwa 'kuhujumu taasisi za kidemokrasia nchini Liberia kwa manufaa ya kibinafsi'. George Weah, ambaye alikuwa amefanya vita dhidi ya ufisadi kuwa moja ya vipaumbele vyake vikuu, amelazimika kujitenga na maafisa hao katika serikali yake.

Katika tovuti ya serikali ya Liberia, Rais George Weah amesema ana wasiwasi na madai ya Wizara ya Fedha ya Marekani, ambayo iliwabana washirika wake watatu wa karibu kwa vitendo vya rushwa. Maafisa wakuu waliowekewa vikwazo na Marekani wanajulikana vema: kuna Nathaniel McGill, mkurugenzi katikaofisi ya rais wa Jamhuri, Sayma Syrenius Cephus, mwanasheria mkuu, na Bill Twehway, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya kitaifa.

George Weah alitaja madai hayo ya Marekani kuwa "mazito". Kutokana na hali hiyo, aliwasimamisha kazi "mara moja" watu hao watatu aliowataja, kabla ya kuwabadilisha na manaibu wao, muda wa kufanya uchunguzi. Kwa mujiu wa mwandishi wa habari wa Liberia Bettie Mbayo, mkuu wa nchi hakuwa na chaguo jingine:

“Huwezi kusema unataka kupigana na ufisadi wakati huo huo washirika wako wa karibu wanawekewa vikwazo baada ya kudhihirika kuwa wanajihusisha na kashfa hiyo. Hii inazua maswali waziwazi kuhusu uadilifu wa George Weah. Sasa ana wajibu wa kuonyesha kwamba yeye ni mkweli kuhusiana na ahadi zake. »

Mnamo 2017, mwaka wa kuchaguliwa kwake, Rais Weah aliweka vita dhidi ya ufisadi kuwa kipaumbele chake. Lakini tangu wakati huo, hakuna kinachoendelea. Wakati upinzani wa Liberia unakaribisha kusimamishwa kazi kwa maafisa watatu wakuu, mtafiti Ibrahim Al-Bakri Nyei anaomba marekebisho ya kimuundo:

“Dau ni muhimu zaidi kuliko kufukuzwa kwa watumishi wa umma. Ni suala la uwezo, uadilifu na uhuru wa taasisi za Liberia. Ikiwa serikali ya kigeni itakuambia kuwa serikali yako ni fisadi na inakufanyia kazi, hiyo inamaanisha kuwa hauongozi serikali inayofanya kazi. »

Vikwazo hivyo vya Marekani vilivyotangazwa Jumatatu vinakuja mwezi mmoja baada ya George Weah kuialika Washington kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika, ambapo vita dhidi ya ufisadi vinapaswa kujadiliwa. Mkutano huo utafanyika kuanzia Desemba 13 hadi Desemba 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.