Pata taarifa kuu

Kiongozi wa waasi wa Liberia Kunti Kamara ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Akihukumiwa mjini Paris kwa mauaji na dhulma zilizofanywa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia, kiongozi wa zamani wa waasi wa kundi la Ulimo, Kunti Kamara alitangazwa Jumatano hii, Novemba 2 kuwa na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Katuni iliyotengenezwa Oktoba 10, 2022, ikimuonyesha aliyekuwa kamanda wa kundi la Ulimo Kunti Kamara, katika Mahakama ya Paris.
Katuni iliyotengenezwa Oktoba 10, 2022, ikimuonyesha aliyekuwa kamanda wa kundi la Ulimo Kunti Kamara, katika Mahakama ya Paris. AFP - BENOIT PEYRUCQ
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki tatu Mahakama ya Paris ikishughulikia kesi kuhusiana na  vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia vilivyoambatana na ukatili, hatimaye imetoa uamuzi wake siku ya Jumatano kuhusu kamanda wa zamani wa waasi Kunti Kamara, ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Kwa maneno yake ya mwisho mahakamani, mshtakiwa, mwenye upara na masharubu mengi, alipinga shutma dhidi yake Jumatano asubuhi. "Sina hatia leo, sina hatia kesho, nilikuwa askari wa kawaida tu," alisema Kunti Kamara.

"Uhalifu uliofanywa ni wa kutisha sana kuelezeka," alisemambele ya majaji mwandishi wa habari na mwanaharakati wa Liberia John Stewart.

Wakati wa vita vya kwanza kati ya viwili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia (1989-1997), Kunti Kamara alikuwa mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vuguvugu la Ukombozi wa Demokrasia (Ulimo), ambalo lilikuwa limechukua eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi na kuzuia wanamgambo wa Charles Taylor. Ni katika eneo hili la Lofa ambapo "C.O Kundi" - kwa "afisa mkuu" - alishiriki katika mauaji dhidi ya raia ambao umemfanya afikishwe mahakamani huko Paris tangu Oktoba 10, kwa niaba ya mamlaka ya ulimwengu inayotekelezwa na Ufaransa kwa uhalifu mkubwa zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.