Pata taarifa kuu
LIBERIA-HAKI

Mahakama ya Liberia yatupilia mbali mashtaka dhidi ya mpinzani wa Rais Weah

Mahakama nchini Liberia imetangaza kuondolewa kwa mashtaka dhidi ya Henry Costa, mpinzani wa serikali na mwanahabari, ambaye ataweza kurejea nchini humo.

Henry Costa ni mmoja wa waanzilishi wakuu wa maandamano yaliyoandaliwa Januari 2020 dhidi ya Rais Weah, ambaye upinzani unamtuhumu kwa kushindwa kuiweka kiuchumi nchi hii maskini.
Henry Costa ni mmoja wa waanzilishi wakuu wa maandamano yaliyoandaliwa Januari 2020 dhidi ya Rais Weah, ambaye upinzani unamtuhumu kwa kushindwa kuiweka kiuchumi nchi hii maskini. RFI/Darlington Porkpa
Matangazo ya kibiashara

Bw. Costa, ambaye ni mtangazaji wa kipindi maarufu cha redio kutoka Marekani, ni mpinzani mkubwa na mkosoaji wa Rais George Weah, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa soka ambaye ni rais tangu mwaka wa 2018.

Mtangazaji huyo wa redio pia ni mmoja wa waanzilishi wakuu wa maandamano yaliyoandaliwa Januari 2020 dhidi ya Rais Weah, ambaye upinzani unamtuhumu kwa kushindwa kuiweka kiuchumi nchi hii maskini.

Mnamo mwezi Oktoba 2019, mamlaka ya Liberia ilifunga kituo cha redio cha Roots FM, kituo cha redio cha mkosoaji wa Rais Weah, kilichotuhumiwa kuchochea vurugu na kuchota pesa kutoka kwa Waliberia kwa kuwatishia kwa matusi.

Mwanahabari huyo alikuwa amerejea nchini mwake na kupokelewa na umati mkubwa wa watu mwishoni mwa mwaka 2019, katikati ya maandamano ya kumpinga Weah. Bw. Costa alikuwa akichunguzwa na mamlaka ya Liberia ambayo ilisema ilishuku kuwa hati zake za kusafiri zilighushiwa.

Bw. Costa alikuwa akichunguzwa na mamlaka ya Liberia ambayo ilisema ilishuku kuwa hati zake za kusafiri zilighushiwa.
Bw. Costa alikuwa akichunguzwa na mamlaka ya Liberia ambayo ilisema ilishuku kuwa hati zake za kusafiri zilighushiwa. RFI/Darlington Porkpa

Baada ya matatizo na idara ya uhamiaji ya Liberia, mahakama ilimwamuru aripoti mara kwa mara kwa mamlaka, lakini Bw. Costa aliamua kuondoka Liberia kupitia njia za panya mapema mwaka 2020. Baada ya kuzuiliwa kwa muda katika nchi jirani ya Sierra Leone, aliweza kurudi Marekani.

Wizara ya Sheria ilitangaza Alhamisi jioni katika taarifa kwa vyombo vya habari kufutwa mara moja kwa kesi dhidi ya mpinzani huyo. Pia iliamuru kurejeshwa kwa vifaa vyake vya utangazaji ambavyo vilikamatwa. Hatimaye, wizara ilimwalika Bw. Costa kurudi Liberia ili "kuishi kwa uhuru kama raia mwingine yeyote".

Hata hivyo, taarifa hiyo ilimuonya dhidi ya kueneza taarifa potofu na kumtaka kutii sheria.

"Wizara haitakaa kimya na kuruhusu mtu yeyote kuteka nyara au kuchukua nafasi ya kidemokrasia kwa uwongo, uvumbuzi na habari potofu kwa sababu za ubinafsi," wizara hiyo imesema. Bwana Costa alikaribisha habari hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Liberia, iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua takriban watu 250,000 kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2003, na kukumbwa na virusi vya Ebola (2014-2016), inapambana na mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu yake. Waandishi wa habari nchini Liberia, nchi yenye watu milioni tano, mara kwa mara wananyanyaswa au kutishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.