Pata taarifa kuu
LIBERIA-UHURU

Liberia yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 200 tangu kuundwa kwake kama taifa huru

Liberia iliadhimisha Jumatatu hii, Februari 14, mwaka wa 200 tangu kuwepo kwake. Nchi hiyo iliwapokea viongozi na watu mashuhuri kadhaa wa kigeni kuadhimisha kuwasili, karne mbili zilizopita, kwa watumwa wa kwanza walioachiliwa huru kutoka Marekani.

Kitongoji cha West Point huko Monrovia, Liberia.
Kitongoji cha West Point huko Monrovia, Liberia. JOHN WESSELS AFP
Matangazo ya kibiashara

Bendi za muziki na ngoma za kitamaduni ziliburudisha siku hiyo katika uwanja wa soka wa Samuel Doe uliojaa watu wengi huko Monrovia. Raia wa Liberia walimiminika katika uwanja huo kushiriki katika sherehe hizo. Miongoni mwa wageni, marais wa Gambia, Niger na Togo pamoja na wawakilishi wa Nigeria, Gabon na Marekani.

Ni wakati wa kihistoria, kulingana na Rais George Weah ambaye alifungua sherehe za maadhimisho ya miaka mia mbili. "Leo tunaadhimisha miaka 200 tangu kuanza kwa safari yetu ya kuwa taifa huru, na hatimaye kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuanzishwa kama taifa huru."

Wakati watumwa wa kwanza huru wa Kimarekani walipofika mwaka wa 1822 katika eneo hili lililoitwa Monrovia, uhusiano na wakazi wa eneo hilo ulifika unakuwa mgumu mara moja. N hali hiyo nio chimbuko la vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mara mbili, ambavyo vilisababisha vifo vya watu 250,000. Rais George Weah, alitaka kusisitiza juu ya umoja wa kitaifa .

"Lazima tujikite katika kukuza umoja miongoni mwa Waliberia wote na kuhimiza kila mtu kutoa michango ya maana katika ujenzi wa taifa letu," alisema. Ninaamini kwamba mababu zetu watatazama Liberia ya leo kwa fahari na kuridhika, kuona ndoto zao zikitimia. »

Lakini ukweli ni tofauti na yanayozungumzwa. Liberia, nchi yenye takriban watu milioni 5 inayopatikana kwenye pwani ya Atlantiki, inasalia kuwa mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.