Pata taarifa kuu

Liberia: Watu 29 wafariki katika harakati za umati kwenye mkusanyiko wa kidini

Takriban watu 29 walifariki Jumatano usiku katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia, wakati umati wa watu ulipojitikeza wakati wa mkutano wa kidini wa Kikristo kwenye uwanja wa soka, polisi imesema.

Rais wa Liberia George Weah akizuru hospitali baada ya tukio la watu kukanyagana katika kanisa moja huko huko Monrovia, lililosababisha vifo kadhaa, Liberia Januari 20, 2022.
Rais wa Liberia George Weah akizuru hospitali baada ya tukio la watu kukanyagana katika kanisa moja huko huko Monrovia, lililosababisha vifo kadhaa, Liberia Januari 20, 2022. via REUTERS - REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

"Watoto walioshiriki katika vita hivi vya msalaba", jina lililopewa mkusanyiko wa aina hii, ni miongoni mwa waathiriwa, msemaji wa polisi Moses Carter ameliambia shirka la habari la AFP.

Ameongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa idadi ya watu katika tukio hili ikaongezeka. "Idadi (ya vifo) inaweza kuongezeka kwa sababu watu wengine wako katika hali mbaya," amesema.

Sababu za mkasa huo hazijulikani.

Vyombo vya habari vya nchini Liberia vimeripoti kwamba waumini walishambuliwa na majambazi, na kusababisha hofu.

Tukio hilo lilitokea wakati wa mkusabyiko wa siku mbili katika wilaya maskini ya New Kru, katika viunga vya mashariki mwa mji mkuu. Mkutano wa maombi karibu na mhubiri maarufu, Mchungaji Abraham Kromah, ulivutia umati mkubwa wa waumini, kulingana na picha zilizotolewa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Mikusanyiko kama hii, huwa ikifanyika katika nchi hii ya kidini na yenye Wakristo wengi, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, iliyoathiriwa sana katika historia yake ya hivi karibuni.

Mwishoni mwa mkusanyiko huo, waumini waliombwa kutoa sadaka kabla ya kuondoka, shahidi mmoja amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.