Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Mauritania: Chama tawala chathibitisha ushindi wake wa kishindo katika duru ya pili

Nchini Mauritania, kumekuwa kumesalia viti 36 pekee vya kujazwa huko mikoani katika duru ya pili ili kuwa na jumla ya muundo wa bunge la kitaifa, hatimaye zoezi hilo limekamilika. Kwa mujibu wa matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge uliotangazwa Jumapili saa kumi na moja jioni na Tume ya Uchaguzi: chama tawala cha El Insafe, ambacho tayari kilikuwa kimeshinda viti 80 katika duru ya kwanza kati ya 176, kimepata ushindi mkubwa.

Kituo cha kupigia kura huko Nouakchott mnamo Mei 13, 2023 wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge.
Kituo cha kupigia kura huko Nouakchott mnamo Mei 13, 2023 wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge. AFP - MED LEMINE RAJEL
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Nouakchott, Léa Breuil

Chama tawala kitakuwa na wingi wa kura katika Bunge. Kulingana na matokeo ya duru ya pili, El Insafe imepata viti vingine 27. Sasa itakuwa na viti 107 kati ya viti 176 bungeni.

Upinzani, kwa upande wake, ambao ulikuwa umepata viti 24 pekee katika duru ya kwanza, umepata viti vingine vitatu, vikiwemo viwili vipya vya chama cha Kiislam cha Tawassoul ambacho kwa jumla kitakuwa na wabunge kumi na moja Bungeni. Kuhusu muungano mpya wa FRUD, umeshinda kiti kimoja na sasa unakuwa na viti saba.

Hakuna mbunge mpya, hata hivyo, kwa upande wa muungano wa SAWAB-RAG ambao Biram Dah Abeid, anayepinga utumwa, alijiunga nao. muungano huo unasalia na viti  5.

Vyama vilivyo karibu na wengi, kambi ya rais, vinashiriki viti 42 vilivyosalia.

Mwaka huu, wanawake wamepata chini ya robo tu ya Bunge la kitaifa (24.2%), ambayo ni zaidi kidogo kuliko mwaka wa 2018.

Matokeo haya bado yatalazimika kuthibitishwa na mamlaka ya juu ya mahakama baada ya kukagua rufaa zinazowezekana. Tume ya Uchaguzi pia inabaini kwamba waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 64.5 katika duru ya pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.