Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Mauritania: Wanajihadi watatu waliotoroka jela waliuawa wakati wa kukamatwa kwao (serikali)

Wanajihadi watatu waliotoroka jela nchini Mauritania siku ya Jumapili Machi 5 waliuawa na wa nne kukamatwa kaskazini mwa nchi wakati wa operesheni ambapo askari mmoja pia aliuawa, serikali ilitangaza Jumamosi Machi 11, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Vue aérienne de Nouakchott, Mauritanie.
Vue aérienne de Nouakchott, Mauritanie. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Wanajihadi hao wanne, akiwemo Mmauritania Saleck Ould Cheikh Mohamedou, anayejulikana kuwa hatari na kuhukumiwa kifo, walikuwa wametoroka jela huko Nouakchott.

Wawili kati yao walikuwa wamehukumiwa kifo, na wengine wawili walikuwa wakisubiri uamuzi wa mahakama kuhusu uhusiano wao na kundi la kigaidi, kulingana na afisa wa jeshi ambaye aliomba kutotajwa jina lake. 

Awali chanzo hicho kilisema kwamba gari lao lilipatikana kaskazini mashariki mwa Nouakchott. Adhabu ya kifo haijatumika tangu mwaka 1987 nchini Mauritania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.