Pata taarifa kuu
IBADA YA HIJA

Waislamu wa Afrika wakaribisha kuondolewa kwa vikwazo vya kuhiji Makka

Saudi Arabia ilitangaza Jumatatu (tarehe 9 Januari) kwamba haitaweka kikomo cha idadi ya mahujaji mwaka huu kwa ajili ya ibada ya Hija iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni. Pia kumeondolewa kikomo cha umri wa miaka 65 kilichowekwa wakati wa mzozo wa UVIKO. Hatua hizi ni afueni kwa waumini wengi hasa barani Afrika.

Waislamu wakisali katika Msikiti Mkuu wakati wa ibada ya kila mwaka ya 'Hija' katika mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia Agosti 8, 2019.
Waislamu wakisali katika Msikiti Mkuu wakati wa ibada ya kila mwaka ya 'Hija' katika mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia Agosti 8, 2019. REUTERS - Waleed Ali
Matangazo ya kibiashara

♦ Nchini Côte d'Ivoire, ambapo idadi ya mahujaji imepungua kutoka 9,000 hadi 4,527 kutokana na mgogoro wa kiafya, kuondolewa huku kwa vikwazo kunaonekana kama kurejea kwa hali ya kawaida.

Ni hisia ya furaha. Mama yangu hakuweza kufanya safari mwaka jana, ilikuwa mshtuko kwake, kwa sababu alikuwa amechanjwa, pasipoti, pesa zilikuwepo ... Kwa bahati mbaya, hakuweza kufanya safari kwa sababu ya umri wake. Kwa hiyo, niliposikia kuhusu hilo, nilijiambia kwamba mwaka ujao, anaweza kwenda.

Mahujaji wa Côte d'Ivoire na mashirika ya usafiri wameelezea furaha yao baada ya kuondolewa kwa kikomo hiki.

♦ Nchini Mauritania pia, waumini wamekaribisha kusitishwa kwa vikwazo vya hajj. Wengine tayari wanajiandaa kwa safari kubwa ya kwenda kuhiji Maka mwaka huu.

"Bila shaka, nimefurahi sana. Miaka ya UVIKO ilikuwa ngumu kwa Waislamu wote wa Mauritania au wa kigeni wanaoishi Mauritania. Tusisahau: wageni wengi wanaoishi Mauritania, hufanya 'Hija' kutoka hapa. Tumefurahishwa na uamuzi uliochukuliwa na mamlaka ya Saudia. Tunamshukuru Mungu, " amesema mmoja wa waumini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.