Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mauritania: Wanajihadi wanne watoroka jela, maafisa wawili wa polisi wauawa

Wanajihadi wanne walitoroka Jumapili jioni jela huko Nouakchott nchini Mauritania baada ya kuwauwa maafisa wawili wa polisi. Mauritani imekuwa tulivu tangu mashambulizi ya mwaka 2011.

Wizara ya Mambo ya Ndani, huko Nouakchott, Mauritania, mnamo Desemba 1, 2022.
Wizara ya Mambo ya Ndani, huko Nouakchott, Mauritania, mnamo Desemba 1, 2022. © RFI / Steven Jambot
Matangazo ya kibiashara

"Saa tatu usiku, Machi 5, 2023, magaidi wanne walifanikiwa kutoroka kutoka jela kuu baada ya kuwajeruhi walinzi, hali ambayi ilisababisha urushianaji riasi kati ya walinzi na wanajihadi hao, na kusababisha vifo vya maafisa wawili wa polisi kupoteza maisha, Wizara ya mambo ya ndani imesema katika taarifa. Majina ya wanajihadi hawa hayajatangazwa.

Wawili kati yao walikuwa wamehukumiwa kifo, na wengine wawili walikuwa wakisubiri uamuzi wa mahakam kuhusu huhusiano wao na kundi la kigaidi, kulingana na afisa wa jeshi ambaye aliomba kutotajwa jina lake. Chanzo hicho kimesema kwamba gari lao limepatikana kaskazini mashariki mwa Nouakchott. Adhabu ya kifo haijatumika tangu mwaka 1987 nchini Mauritania.

"Kikosi cha walinzi wa kitaifa kimeimarisha udhibiti katika gereza hilo na wameanz kufuatilia wanajihadi hao waliotoroka ili kuwazuia haraka iwezekanavyo," pia imebainisha wizara hiyo, ambayo imewataka raia kutoa habari yoyote ambayo inaweza kuchangia kukamatwa kwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.